China ya ongeza matumizi yake katika sekta ya kijeshi.
Beijing, China - 04/03/09. China imeongeza matumizi yake katika sekta ya kijeshi kufikia kiasi cha US $ 70.24 billion, ili kudumisha hali ya ulinzi na usalama.
Kwa mujibu wa msemaji wa serikali, Li Zhaoxing alisema, China haita leta hali ya hatari na wala kutishia nchi yoyote,kwani matumizi hayo ni kwajili ya Wachina na usalama wao.
Kufuatia hali ya China, kuongeza matumizi yake katika fani ya kijeshi, kunafuatia repoti iliyo tolewa na serikali ya Amerika ya kuwa China inaongeza matumizi yake kwenye sekta za kijeshi,hivyo inatakiwa kuwa wazi .
Picha hapo juu wanaonekna wanjeshi wa China, wakiwa wanakula kwata, kati ya moja ya sherehe za kitaifa.
Rais, Abbas na Bi Hillary Clinton, wakutana mjini Ramallah.
Ramallah,Palestina - 04/03/09.Rais wa mamlaka ya Palestina , Mahamoud Abbas,amekutana na waziri wa mabo ya nchi za nje wa Amerika, Bi Hillary Clinton.
Katika mkutano hu uliofanyika mjini Ramallah,Bi Hillary Clinton,alisema ya kuwa serikali ya Amerika ina muunga mkono rais Abbas,na serikali yake ndiyo inayo tambulika, na hivyo Amerika itajitahidi kwa kila hali kuleta amani, na kufikia lengo la kuwa na taifa la Wapalestina watakao ishi jirani na taifa la Izrael.
Picha hapo juu wanaonekna, rais wa taifa la Palestina, Mahamoud Abbas kulia huku akiwa anatabasamu na kwa upande wa kushoto, ni waziri wa mambo ya nchi za nje wa Amerika, Bi Hillary Clinton, wakati walipo kutana mjini Ramallah kujadili hali halisi ya eneo hilo.
Rais wa Sudan atakiwa akamatwe" Hii ni mara ya kwaza kwa rais wa nchi kushitakiwa akiwa madarakani".
Den Haag, Uhollanzi - 04/03/09.Mahakama ya kushughulikia kesi za makosa ya kimataifa, imetoa kibali cha rais wa Sudan Omar Al Bashir, akamatwe ili kujibu mashitaka.
Kwa mujibu wa masemaji wa mahakama hiyo, rais Al Bashir, anakabiliwa na makosa ya kukuika haki za binadamu, na kuhusika kutokuwa na hali ya usalama kwenye eneo la Darfur, ambalo ni moja ya jimbo la nchi ya Sudan.
Hata hivyo ,serikali ya Sudan, imesema haitambui kibali hicho cha kukamatwa kwa rais Al bashir, na haitashirikiana na mahakama hiyo.
Picha hapo juu anaonekana rais wa Sudan, Omar Al Bashir, akisalimia wananchi, wakati akiwa katika ukaguzi wa maendeleo ya nchi hivi karibuni.
Wednesday, March 4, 2009
Rai wa Sudan atakiwa akamatwe"Hii ni mara ya kwanza kwa rais wa nchi kushitakiwa akiwa madarakani".
Posted by
Kibatala
at
Wednesday, March 04, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment