Monday, March 22, 2010

Serikali ya rais Obama ya weka historia.

Serikali ya rais Obama ya weka historia

Washington Amerika - 22/03/2010. Bunge la Amerika limepiga kura kukubali kuanzishwa kwa bima ya afya kwa wanchi wa Amerika, amabo wengi wao walikuwa wanishi bila kuwa na bima za afya.
Katika upigaji huo wa kura wabunge wa cham cah Demokrasi waliwashinda wabunge wa chama cha Republikan kwa kupiga kura zipatazo 219 kwa 212. Wabunge wapatao thelathin na nne wa
chama cha demokras walipinga mswada huo.
Kupita kwa kura hiyo, ambako kulikuwa kunaleta mvutano wa kisiasa kati ya vya hivyo viwili, kutamrahisishia rais Baraka Obama, kuendelea na shughuli nyingine za kitaifa na za kimataifa.
Rais Baraka Obama, anatarajiwa kusaini mswada huo wa bima ya afya kwa wote muda simrefu.
Picha hapo juu anonekana rais wa Amerika, Baraka Obama akiongea kuhusu swala zima la afya kwa wote, huku kushoto ni makamu wa rais Joe Biden akisikiliza kwa makini.
Picha ya pili wanaonekana waganga na wauguzi wakiwa mbele ya bunge kuunga mkono wa mswada wa bima ya afya kwa wote kabla ya kupigwa kura hiyo ya bima kwa wote.

No comments: