Saturday, March 13, 2010

Kanisa Katoliki lakumbwa na kashfa nyingine nchini Ujeruman

India na Urussi kushirikiana katika kuendeleza nguvu za kinyuklia. New Delhi, India - 13/03/2010. Serikali ya India na Urussi zimetilia sahihi mkataba wa kuanzisha ujenzi wa mitambo ya nguvu za nyuklia nchini India. Mkataba huo ulifanyika jiji Delhi wakati waziri mkuu wa Urussi, Vladimir Putin alpo tembela nchini India. Akiongea kuhusu mkataba huo waziri mkuu wa Urussi, Vladimir Putin alisema" tunajenga uhusiano na India hasa katika sekta ya Nyuklia." Naye waziri mkuu wa India Manmohan Singh, alisema " uhusianowetu na Urussi ni wa uhakika katika nyanja tifauti." Picha hapo juu wanaonekana waziri mkuu wa Urusi, Vladimir Putin kushoto akiongea na waziri mkuu wa India Manmoham Singh kulia wakati walipo kutana jijini Delhi hivi karibuni. Kanisa Katoliki lakumbwa na kashfa nyingine nchini Ujeruman. Munich, Ujeruman -13/03/2010. Askofu mkuu wa Kanisa Katoliki nchni Ujerumani ameomba masamahaa kwa niaba ya kanisa kutokana na matukio na matendo yaliyo tokea miaka ya nyuma. Askofu,Robert Zollitsch,aliyasema" Kanisa lita yafanyia uchunguzi madai yote, litawapatia huduma za kiushauri wale wote walioathirika na matukio hayo." Kuomba msamaha huo kunakuja baada ya Kanisa Katoliki kukumbwa na kashfa shutuma kubwa kufuatia malalamiko yaliyo letwa na watu ambao waliathilika na matukio hayo yaliyo tokea ndani ya Kanisa Katoliki. Picha hapo juu anaonekana, Askofu Mkuu Robert Zolliisch akiongea kuhusu matukio yaliyo toke ndani ya kanisa.

No comments: