Sunday, March 21, 2010

Waziri mkuu wa Irak ataka kura zihesabiwe upya.

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa atemelea Gaza.

Gaza, Palestina - 21/03/2010. Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon amefanya ziara katika maeneo ambayo wanaishi Wapalestina hivi karibuni na kudai ni lazima kuwepo na matifa mawili kati ya Waizrael na Wapalestina. Akiongea, katibu huyo wa umoja wa mataifa alisema"kitendo cha Izrael kuzuia misaada kupelekwa kwa Wapalestina si cha haki, kwani kinasababisha maafa makubwa." "Umoja wa mataifa utafanya kila jitihada kuhakikisha wanchi wa Palestina wana kuwa na taifa lao" na kuagiza kuachiwa kwa askari wa Izrael Gilat Shilad aliyekamtwa mwaka 2006. Picha hpo juu anaonekana katibu mkuu wa umoja wa mataifa katikati akiwa anaangalia hali halisi ya Gaza na vitongoji vyake hivi karibuni. Ayatollah azilaumu nchi za Amerika na Izrael.
Tehran, Iran - 21/03/2010. Kiongozi mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamemei
amezilaumu Amerika na Izrael kwa kutaka kuleta machafuko na kuondoa serikali ya Kiislaam ya nchi hiyo. Akiongea katika kusherekea sikukuu ya Nowruz, alisema " Iran ilikuwa katika hali ngumu hata watu kumwaga damu, kwa sababu ya upinzani uliokuwa ukisaidiwa na nchi hizo." Adui walitaka kuigawa nchi yetu na kutak kuleta vita, lakini taifa zima lilisima imara," aliongezea. Picha hao juu anaonekana kiongozi mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, ndiye kiiongozi mkuu mwenye mwenye madaraka ya juu zaidi. Waziri mkuu wa Irak ataka kura kuhesabiwa upya.
Baghdad, Irak, 21/03/2010. Waziri mkuu wa Irak ameagiza kamati inayo shughulikia na kusimamia uchaguzi nchini Irak kuhesabu upya kura. Akiongea waziri mkuu Nouri al Marik, alisema "ni muhimu kufanya hivyo, ili kuleta amani ya kisiasa." Matokea ya uchaguzi ambayo mpaka sasa hayajamalizika kuhesabiwa, yanaonesha chama cha waziri mkuu Nouri al Malik kipo nyuma, ya cha cha mpinzani wake Iyad Alawi. Picha hapo juu anaonekana, waziri mkuu wa Irak, Nouri al Malik akiongea kuhusu swala la uhesabuji wa kura upya. Rais wa Sudan,atakiwa kusafisha jina lake kabla ya uchaguzi.
Kartoum, Sudan - 21/03/2010.
Kiongozi mmoja wa chama cha upinzani cha sudan People's Liberation Movement(SPLM) nchini Sudan, amesisitiza yakuwa rais wa sasa wa Sudani lazima akajibu mashitaka yanayo mkabili katika mahakama ya kimataifa ya Hague iliyopo nchini Uhollanzi.
Akiongea kwa nyakati tofauti, na kukiwa kumebakia siku chache kabla ya uchaguzi wa kuchagua wabunge, Edward Lino, alisema " Hatukumwambia au kushirikiana wakati anafanya hayo makosa na hatukukubaliana naye kwa hilo, hivyo nilazima asafishe jina lake kabla ya kugombe kiti cha urais tena."
Edward Lino aliyaongea hayo wakati wa mkutano wa kuchangia pesa za kujenga upya maeneo yaliyo alibiwa vibaya kutokana na vita.
Picha hapo juu anaonekana rai wa Sudan, Omar al Bashir, ambaye amekuwa akishitumiwa na jumuiya ya kimataifa kutokana na hali mbaya ya Darfur.

No comments: