Friday, March 26, 2010

Kanisa Katoliki " Vyombo vya habari vinachafua jina la Kanisa."

Kanisa Katoliki "Vyombo vya habari vinanchafua jina la Kanisa." Vatican, Vatican City - 26/03/2010. Msaidi wa Papa Benedikt XVI amelaumu vyombo vya habari kwa kujaribu kuharibu jina na kuchafua Kanisa Katoliki na uongozi wake. Akiongea baada ya habari kutolewa ya kuwa Papa Benedict wakati akiwa Kadinali alifutilia mbali malalamiko yaliyoletwa ya kuwa baadhi ya mapadri walikuwa wananyanyasa waumini kijinsia "yanalengo la kuaribu Kanisa na uongozi wake." Kanisa Katoliki limekuwa na wakati mgumu baada ya waumini na wanafunzi waliosoma katika shule za Kanisa hilo kulalamika ya kuwa walinyanyaswa kijinsia wakati wakiwa masomoni katika shule hizo. Picha hpo juu anaonekana Papa Benedikt VXI, akiwasalimia waumini waliokuja kusali na kuomba Mungu kwa pamoja katika moja ya sikuku za Kikristu ndani ya la jiji Vatican. Nchi za Kiaarabu kuchanga pesa kuwasaidia Wapalestina. Sirte, Libya - 26/03/2010. Mawaziri wa mabo ya nchi za nje wa nchi za Kiarabu wamekubaliana kutoa na kuchangisha kiasi cha $500million kwaajili ya kuwasaidia Wapalestina wanao ishi Jerusalem. Mawaziri hao wanaokutana kabla ya mkutano mkuu wa wakuuwa nchi za Kiarabu, umesema "mchango huyo ni kwaajili ya kukabiliana na ujenzi ambao unaendelea katika eneo hilo la Jeruusalemu. Picha hapo juu wanaonekana mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Kiaarabu wakiwa katika kikao katika mti wa Sitre. Iyad Alawi ashinda uchaguzi wa Irak.

Baghdad, Irak 26/03/2010. Kamati inyosimamia uchaguzi nchini Irak imetangaza chama cha Irakiya Coalition kimeshinda katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni.
Chama hicho kinacho ongozwa na aliyekuwa waziri mkuu wa zamani wa Irak, Ayad Allawi, kimepata viti 91 katika bunge la Irak na chama cha waziri mkuu wa sasa ANour al Malik kimeshinda viti 89.
Hata hivyo ili kuunda serikali Ayad Allawi, itambidi atafute chama shiriki jambo ambalo wataalamu wa siasa ya Irak wanasema " itabidi afanye kazi ya ziada, kwa kufuatia historia ya uongozi wake wa nyuma."
Picha hapo juu, anaonekana Ayad Allawi akiongea wakati wa kampeni za uchaguzi.

No comments: