Sunday, March 14, 2010

Rais wa Zimbabwe aunga mkono chama cha Consevertive.

Rais wa Zimbabwe aunga mkono cham cha Consevertive.

Harare, Zimbabwe - 14/03/2010. Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, ameunga mkono mabadiliko ya uongozi wa kisiasa nchini Uingereza kwa kusema "ni vizuri uongozi wa chama cha Conservative kinachoongozwa na David Cameron kushinda uchaguzi ujao, kwani tunaweza kushirikiana na kuelewana nao, kuliko Labour ambao viongozi wake ni waaoga kukutana na sisi."
Rais Mugabe , alikuwa akijibu maswali baada ya ziara ya rais wa Afrika ya Kusini Jakob Zuma aliyoifanya hivi karibuni nchni Uingereza na kuongelea swala la kuondolewa vikwazo kwa serikali ya Zimbabwe.
Hapo juu anaonekana rais wa
Somalia kupata msaada wa kijeshi.
Moghadishu, Somalia - 14/03/2010. Serikali ya Somalia inajiandaa kijeshi kukabiliana na makundi ya kijeshi yaliyopo nchini humo ambayo yame uteka mji mkuu wa Mogadishu.
Kwa mujibu wa habari zilizo tolewa na mmoja wa mkuu wa majeshi ya Somali alisema " Misaada ya kijeshi itapatikana na mingi kutoka Amerika"
Hata hivyo serikali ya Amerika ilikanusha habari hizo
Washington imekuwa ina tafuta ni njia gani itaweza kuleta amani katika eneo hilo ambapo inaminika kundi la Alqaeda lina wafuasi wake.
Picha hapo juu ni baadhi ya wapiganaji wakiwa katika doria jiji Mogadishu.
Pesa yetu itabaki katika mzunguko wa kawida.
Beijing, China - 14/03/2010. Serikali ya China imesema yakuwa lawama zinazo tolewa na baadhi ya nchi kuhusu hali ya kibiashara na mzunguko wa fadha wa China ni wa bure kwani nchi hizo zinataka hali nzima iwe kwa faida ya mataifa yao kibiashara na kiuchumi.
Akiongea katika mkutano waziri mkuu wa China, Wen Jiabao, kuhusu mvutano uliotokea kati ya Beijing na Washingtone siku ya Alhamisi kuhusu swala zima la biashara na mzunguko wa fedha kwa kusema"China itaweka mzunguko wa pesa zake katika hali ya kawaida, ijapokuwa Amerika imedai mabadiliko yafanyike"
Picha hapo juu anaonekan waziri mkuu wa China, Wen Jiabao akiwasalimia walioudhulia mkutano jijini Beijing.

No comments: