Thursday, March 18, 2010

Zuma ashinda kura za maoni

Zuma ashinda kura za maoni. Cape Town, Afrika ya Kusini -18/03/1020. Rais wa Afrika ya Kusini ameshinda kura za maoni ambazo zilikuwa zimepigwa hivi karibuni, baada ya vyama vya upinzani kudai kura hizo zipigwe. Vyama vya Congre of people na Democratic Alliance ndivyo viliongoza kwa kutakura za maoni zipigwe. Kura za maoni zilizo pigwa 241 zili kubali uongozi rais Jakob Zuma, na 81 zilipinga uongozi wake. Kura hizo ni za kwanza tangu Afrika ya Kusini kutoka katika serikali ya kibaguzi mwaka 1994. Picha hpo juu anaonekana rais wa Afrika ya Kusini Jakob Zuma, katikati akiwa anashiriki katika mila na utamaduni wa kabila lake la Zulu ambapo huwa anashiriki kikamilifu bila kuficha. Anyongwa kwa makosa ya kifedha. Pyongyang, Korea ya kaskaziani - 18/03/2010. Serikali ya Korea ya Kaskazini ilimuhukumu kifo na kumyonga afiasa mmoja aneye shughulika na mswala ya fedha na uchumi baada kubainika alikuwa anakwenda kinyume na sheria. Afisa huyo Pak Nam-ki, aliuwawa kwa kupigwa risasi. Hata hivyohabari kutoka Korea ya Kusini zinamsema , kuuwawa kwa bwana Pak kunakuja baada ya kubainika alikuwa anapingana na sera za serikali ya mapinduni ya Korea ya Kusini. Picha hapo juu, ni ya bendera ya Korea ya Kaskazini, nchi ambayo imekuwa ikilaumiwa kwa kukiuka haki za binadamu kila wakati. Kitendawili cha Iran jibu bado kwa Amerika na Urusi.

Moscow, Urusi - 18/03/2010. Waziri wa mabo ya nje wa Amerika, Bi Hillary Clinton, amekutana na waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergey Lavrov, na kuitaka serikali ya Urusi kusimamisha kwa muda kuisaidia Iran kujenga mtambo wa kinyuklia wa Buchehr.
Akiongea bi Haillary Cinton, alisema " Ikiwa Iran itaonyesha ya kuwa ina nia ya kushirikiana kujenga mtambo ambayo aitazalisha siraha za kivita."
Hata hivyo, waziri wa mambo ya nje wa Urusi,Sergy Lavrov, alisema " Ujenzi wa mitambo ya kunyuklia nhcini Iran, utakuwa chini ya uangalizi wa jumuia ya kimataifa."
Kwa mujibu wa mkataba uliopo kati ya Iran na Urusi, utaghalimu kiasi cha million 700 pound.
Picha hapo juu anaonekana Bi Hillary Clinton, akiongea na waandishi wa habari jijini Moscow.

No comments: