Saturday, November 6, 2010

Kikwete aapishwa kuwa rais wa Tanzania kwa miaka mitano mingine.

Kikwete aapishwa kuwa rais wa Tanzania kwa miaka mitano mingine.

Dar es Salaam, Tanzania - 06/11/2010.Watanzania wameshuhudia kuapishwa kwa mara nyingine tena kwa Jakaya Kikwete kuwa rais kwa kipindi kingine cha miaka mitano.
Rais Jakaya Kikwete ambaye alikuwa akigombea kiti hicho cha urais kwa kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) alishinda kura kwa asilimia 61zidi ya wapinzani wake.
Mara baada ya kuapishwa kuwa rais wa nchi Jakaya Kikwete alisema "nitahakikisha wanachi wana kuwa na amani na kukuza uchumi wa nchi."
Picha hapo juu anaonekana rais wa sasa wa Tanzania Jakaya Kikwete akiongea na waandishi wa habari kabla ya kampeni za uchaguzi wa rais wa 2010 kuanza.
Picha ya pili anaonekana rais Jakaya Kikwete akiingia uwanjani tayari kuapishwa kuwa rais wa Tanzania kwa mara nyingine.
Picha ya tatu wanaonekana viongozi wa nchi tofauti walioudhulia sherehe za kuapishwa rais Jakaya Kikwete.
Picha ya mwisho anaonekana rais Jakaya Kikwete akiongea na rais mstaafu Benjamin Mkapa, wakati wa moja ya mkutano ya chama cha Mpinduzi ambacho ni cham tawala.

No comments: