Monday, November 29, 2010

Serikali ya Amerika ya shutumu uchapishwaji wa habari za siri kwenye vyombo vya habari.

Serikali ya Amerika ya shutumu uchapishwaji wa habari za siri kwenye vyombo vya habari. Washington, Amerika - 29/11/2010. Serikali ya Amerika imeshutumu kitendo cha kuchapishwa habari za siri ambazo zimesambazwa kwenye vyombo vya habari tofauti. Akiongea mbele ya waanshishi wa habari, waziri wa mambo ya nchi za nje wa Amerika Hillary Clinton alisema "kitendo hicho ni kibaya na kinahatarisha usalama wa raia katika jumuiya ya kimataifa na maelezo yaote yalio elezwa katika habari hizo siyo msimamo wa serikali ya Amerika na watu wake." Akiongea kwa kusisitiza Hillry Clinton aliendelea kwa kusema kuwa "ushirikiano uliopo kati ya serikali za kimataifa na Amerika utazidi kudumishwa na kushinda kitendo hicho ambacho siyo kizuri cha kusikitisha." Picha hapo juu anaonekana waziri mambo ya nje wa Amerika Hillary Clinton akiongea na waandhishi wa habari kuhusu uchapishwaji wa habari za siri kwenye vyombo vya habari zilizo tolewa na WIKI LEAKS. Serikali ya Iran yazishutumu nchi za Magharibi mara baada ya mauaji ya mwansayansi wake. Tehran, Iran 29/11/2010. Rais wa Iran ameshutumu serikali za magharibi baada ya kutokea mauaji ya mwanasayansi wake wa kinyuklia ambaye ameuawawa na bomu lililo tengwa kwenye gari lake.

Akiongea mbele ya waandishi rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad alisema " hizi ni njama za serikali za magharibi na njama hizi hazitafanikiwa kusimamisha maendeleo ya sayansi ya kinyuklia." Rais wa Iran akiongelea kuhusu kuchapishwa kwa habari za siri za aliseama " habari hizo hazitaisumbua Iran, kwani ni njama za Amerika katika harakati zake za kijasusi na kwa Iran hili hatazitilia maanani na tutaendelea kushirikiana na nchi za jirani kama kawaida kwa habari zilizomo zinania ya kuharibu uhusiano wa Iran na majirani zake."
Picha hapo juu anaonekana rais wa Iran Mahmoud Ahmedinejad akiongea na waandishi wa habari.

No comments: