Sunday, November 28, 2010

Wiki Leaks yaja na habari mpya za kustusha.

Wiki Leaks yaja na habari mpya za kustusha

Washington, Amerika- 28/11/2010. Serikali ya Amerika imekilaani kitendo cha shirika la habari lijulikanalo kama Wiki Leaks kwa kutoa habari za siri kwanye mtandao wake na kusambaza kwa mashirika mengine ya habari.
Kwa mujibu wa habari kutoka Washington zinasema " kitendo cha Wiki Leaks kutoa habari hizo za siri zitahatarisha usalama wa maisha ya jamii.
Hata hivyo mwanzilishi wa shikika hilo Jualian Assange aliema "kutolewa kwa habari hizo kutaleta mabadiliko makubwa katika jamii." "Picha hapo juu anaonekana rais wa Amerika Baraka Obama na kwa nyuma anaonekanaka waziri wa mambo ya nje wa Amerika Hillary Clinton ambapo serikali ya Amerika ina hitahusishwa kwa kiasi kikubwa kwenye habari za siri zilizotolewa na Wiki Leaks.

No comments: