Tuesday, November 2, 2010

Somalia yapata waziri mkuu mpya.

Somalia yapata waziri mkuu mpya.

Mogadishu, Somalia - 02/11/2011. Bunge la serikali ya Somalia limekubali kwa pamoja kumpishatisha waziri mkuu mpya. Mohamed Abdullahi Mohamed ambaye aliteuliwa na rais wa sasa wa Somalia Sharif Sheikh Ahmed mapema 14 Oktoba ili kuchukua nafasi iliyo achwa wazi na waziri mkuu aliyeziudhuru Omar Abdirashid Sharmarke Septemba 21. Akiongea mara baada ya kupitishwa kuwa waziri mkuu wa Somalia, Mohamed Abdillah Mohamed alisema "majukumu yangu ya kwanza ni kupambana na ugaidi ili kuleta usalama kwa Wasomalia." Picha hapo juu anaonekana waziri mkuu mpya wa Somalia Mohamed Abdillah Mohamed akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kuteuliwa na kuchaguliwa kuwa waziri mkuu. Vikwazo vyaendelea kuwekwa zidi ya serikali ya Sudan.
Washington, Amerika - 02/11/2010. Serikali ya Amerika imeendelea kuiwekea vikwazo serikali ya Sudan. Kwamujibu wa habari zilizo patikana zinasema "vikwazo hivyo vinania ya kurazimisha serikali ya Sudani kupitisha swala kura ya maoni ambalo uenda likaigawa nchi hiyo katika sehemu mbili." Picha hapo juu anaonekana mmjoja ya kijana akiwa ndani ya basi akiangalia kitu fulani wakati nchi yake bado inaendelea kuwekewa vikwazo.
Waingereza na Wafaransa watiliana sahii katika maswala ya ulinzi.
London, Uingereza - 02/11/2010. Serikali za Uingereza na Ufaransa zimetiliana mikataba ya maswala ya ulinzi hivi karibuni jijini London. Mikataba hiyo ambayo itaifanya serikali zote kushirikiana kikamilifu katika maswala ya ulinzi wa kinyuklia na ushirikiano wa mambo ya kijeshi kwa ujumla
Mkataba huu ambao ulisainiwa na rais wa Ufaransa Nikolas Sarkozy na waziri mkuu wa Uingereza David Cameron wakati walipo kutana jijini London.
Akiongea mara baada ya kumaliza kutia saini mikataba hiyo ya ulinzi waziri mkuu wa Uingereza alisema "leo tumefungua ukurasa mpya wa ushirikiano katika maswala ya ulinzi kati ya nchi hizi mbili."
Picha hapo juu wanaonekana waziri mkuu wa Uingereza David Cameron kulia akiongea na rais wa Ufaransa Nokolas Sarkozy mara baada ya kutiliana sahii mikataba hiyo.
Waamerika wapiga kura kuwachagua wabunge.
Washington, Amerika - 02/11/2010. Wananchi wa Amerika wameanza kupiga kura kuwachagua wabunge ambapo inasadikiwa matokeo ya uchaguzi huo huenda yakaleta mabadilikio makubwa ya kisiasa kati ya vyama vya Demokratic na Republikan.
Kwa mujibu wa ripoti zilizo patikana zinasema "chama cha Republikan huenda kikapata viti vingi katika bunge,"
Picha hapo juu anaonekana mke wa rais wa Amerika bi Michelle Obama akiwa katika kampeni kuwahamasisha wananchi wapige kura na kupigia chama cha Demokratik.

No comments: