Wednesday, November 3, 2010

Baraka Obama na Demokratik wazidiwa kete na Republikan.

Baraka Obama na Demokratik wazidiwa kete na Republikan.

Washington, Amerika - 03/11/2010. Matokeo ya uchaguzi nchini Amerika yamemalizika nchini Amerika na chama cha Republikan kupata ushindi dhidi ya chama cha Demokratik.
Matokeo hayo ya uchaguzi yameweza kuipa chama cha Republikan kupata viti vingi katika bunge ambapo inaaminika yakuwa matokeo hayo huenda yakampa wakati mgumu rais Baraka Obama katika uongozi wake kwa kipindi kilichobakia.
Akiongea baada ya matokeo hayo rais wa Amerika wa Amerika Baraka Obama alisema " nina wajibika na matokeo yote ya kushindwa kwa uchaguzi kwa chama cha Demokras na hii imeonyesha ni kwa kiasi gani bado wananchi hawajaridhika na juhudi zetu, na hivyo kuna haja ya kuongeza juudi zaidi kufikia malengo ya kuinua uchumi wa Amerika."
Obama aliongezea kwa kusema "pia nitashirikiana kikamilifu na viongozi wa chama cha Republikan ili kuendeleza na kukamilisha malengo ya kuinua uchumi wa Amerika."
Picha hapo juu inaonyesha viti vya bunge na kulia vyene rangi nyekundu ni viti vya wabunge wa chama cha Republikan amba wamepata kura zaidi na kushoto ni viti vya wabunge wa Demokratik ambao wamepoteza kura na viti katika bunge.
Picha ya pili anaonekana rais wa Amerika Baraka Obama wakati wa kampeni cha uchaguzi wa wabunge hivi karibuni.
Picha ya tatu anaonekana Bi Hillary Clinton akisalimiana wa watu akiwa katika kampeni za uchaguzi wa wabunge hivi karibuni.
Izrael kufikiria upya mazungumzo na Uingereza.
Tel Aviv, Izrael - 03/11/2010. Serikali ya Izrael imesema haitafanya mazungumzo na Uingereza kutokana na sheria ambayo inaruhusu mahakama kuwashitaki maafisa wa Izrael ambao watatembelea Uingereza kwa kuhusishwa na makosa ya kivita..
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana zinamsema "nchi hizo mbili huwa zinafanya mazungumzo katika maswala ya ulinzi kila mwaka."
Picha ya kwanza hapo juu ni ya nchi ya Uingereza nchi ambayo ina ushirikiano wa karibu na Izrael.
Picha ya pili ni ya nchi ya Izrael nchi ambayo inaitaka serikali ya Uingereza kubadilisha sheria ambayo ina weza kuwashitaki raia wa Izrael ambao wanashukiwa kuwa na makosa ya kivita.
Rais wa zamani wa Amerika ajianda kutoa kitabu chake.
Washington, Amerika - 03/11/2010. Aliyekuwa rais wa Amerika George Bush anatarajiwa kutao kitabu chake ambacho kiteelezea hali halisi wakati wa uongozi wake mpaka hapo alipo mwachia ofisi rais wa sasa Baraka Obama.
Kwa mujibu wa habari zilizo patikana zinasema rais huyo wa zamani George Bush alisema "huwa wakati mwingine anajisikia vibaya kwa kukuso kuzipata siraha za maangamizi ya jamii ambazo zilikuwa ndiyo kiini cha kuanza kwa vita hivyo."
Picha hapo juu anaonekana rais wa zamani George Bush enzi zake alipokuwa rais wa Amerika kuelekea kuhutubia bunge.

No comments: