Iran yasema yafanikwa kutengenza roketi ya ulinzi.
Tehran,Iran 20/11/2010. Maofisa wa kijeshi wa serikali ya Iran wamedai wamafanikiwa kutengeneza roketi ya kiulinzi na kuifanyia majaribio wakati wa mazoezi ya siku tano ya kijeshi.
Akiongea Brigedia Meja General Mohammad Hassan Mansouria alisema " kwa kutumia maalifa ya wanasayansi wa hapa nyumbani tumeweza kutengeneza roketi kwa jina S-200 ambayo ni kwa ajili ya ulinzi na inauwezo sawa na ile ya Urussi S-300. Akisisitiza zaidi Brigadia huyo alisema katika mazoezi hayo tuliweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa katuika maswala ya ulinzi na mashambulizi ya maadui.
Mazoezi ya kivita ya Irani yalianza siku ya Jumanne kwa madhumuni ya kuangalia ni kwa jinsi gani jeshi hilo tiyali kwa mashambulizi ya aina yoyote.
Picha hapo juu inaonekana moja ya roketi ya Kiiran ikipaakuelekea angani baada ya kulipuliwa wakati wa mazoezi ya kivita ya jeshi la Iran.
Sahara ya Magharibi, Morokko - 20/11/2010. Serikali ya Morokko imetetea kitendo cha serikali yake kuvamia kambi za wananchi ambao wanaishi katika maeneo ya Sahara ya Magharibi na kudai yalikuwa ya kuleta amani.
Lisboa, Ureno 20/11/2010. Viongozi wa NATO wanakutananchini Ureno ili kujadili na kupanga mipango ya kukabidhi maswala ya ulinzi kwa Wananchi wa Afghanistan.
Akiongea wakati waufunguzi wa makutano huo katibu mkuu wa NATO Anders Fogh Rasmussena alisema "mafanikio ya mkutanao huu ni kuhakikisha wananchi wa Afghanistan wanaweza kuongoza na kulinda nchi yao na kukabidhi madaraka yote ya ulinzi kuwa mikononi mwa. na kuendelea kudumisha ushirikiano na wananchi wa Afghanistan."
No comments:
Post a Comment