Wednesday, November 17, 2010

Mamiliioni ya Waislaam washerekea sikukuu ya Hajji

Mamilioni ya Waislaam washerekea sikukuu ya Hajji

Makka, Saud Arabia 17/11/2010.Mamilion ya Waumini wa dini ya Kiislaam wamasherekea siku ya Iddi Al Hajj.
Kuazimisha siku kuu ya Hajj, baadhi ya Waislaam ambao wamejaliwa kwenda Kuhiji Makka huwa wana swali na kumkana shetani na mambo yake yote na kuomba masamaha kwa Mungu muumba wa vitu vyote tuvionavyo na tusivyo viona.
Picha ya kwanza ni ya kitabu Kitukufu Kuraan kitabu ambacho ni nguzo na msingi wa dini ya Kiislaam.
Picha ya pili ni ya Sura ya kwanza ya kitabu Kitukufu Kuraan Surat al Fatiha ambayo ni wajibu wa kila Mwislaam kuitambua.
Picha ya tatu inaonyesha siku ya Hajj ni siku ambayo Waislaam wote huwawana wanashirikiana wa kila kitu ili kuwa karibu na Mungu na katika picha wanaonekana Maelfu ya Waislaam waliokwenda Kuhijji wakiwa wana zunguka Al Kabba kukmilisha Hijja zao.
Rais wa Irak akataa kusaini hukumu ya kifo cha Tari Aziz.
Baghdad, Irak 17/11/2010.Rais wa Irak Jalal Talabani amsema hatasaini ruhusa ya kutaka kunyongwa aliye kuwa waziri wa mambo ya nchi za nje na naibu waziri mkuu Tarik Aziz.
Rais, Jalal Talabani alisema"sita saini kifo cha Tarik Aziz, kwasababu mimi ni mjaamaa na Tarik ni mkristu na ni mzee na najisikia huruma juu yake."
Picha hapo juu anaonekana rais wa Irak, Jalal Talabani akitoka kuzungumza na waandishi wa habari na kuelezea hali halisi ya Irak kwa ujumla.
Tutafanya kazi na wanachi pamoja asema Aung San Suu Kyi.
Rangoon, Myanmar - 17.11/2010.Kiongozi ambaye anatetea demokras nchini Myanmar ana aliye achiwa huru kutoka kizuizini ameomba jumuia za kimataifa kuondoa vikwazo ambavyo vilikuwa vimewekwa zidi ya nchi yake.
Aung San Suu Kyi, ambaye alikuwa kizuizini kwa kipindi cha zaidi ya miaka kumi alisema " Nataka kusikia wananchi wa Myanmar wakisema ya kuwa wanauwezo wa kusema na kufnya vitu kwa maamuzi yao bila woga, na tutafanya kazi ya kuinua maisha ya kila mwananchi, na haki za binadamu zitalindwa na kutekelezwa kisheria."
Aung San Suu Kyi aliyasema hayo mbele ya wanachama wa chama DeNational League for mocracy(NLD) walipo kuja kumlaki mara baada ya kuachiwa kutoka kizuizini.
Picha hapo juu anaonekana bi Aung San Suu Kyi akiwasalimia watu waliokuja kumlaki mara baada ya kuruhusiwa kutoka kizuizini.

No comments: