Saturday, November 27, 2010

Waziri mkuu wa Lebanoni awasili nchini Iran

Waziri mkuu wa Lebanoni awasili nchini Iran.

Tehran, Iran 27/11/2010. Waziri mkuu wa Lebanoni amewasili nchini Iran kwa ziara ya kiserikali. Saad Hariri amewasili nchini Iran ili kudimisha husiano na serikali hiyo. Katika ziara yake Saad Hariri, atakutana na rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejadili kujadili njia za kudimisha ushirikiano wa karibu zaidi. Picha hapo juu anaonekana waziri mkuu wa Lebaboni, Saad Hariri akichuka ndani ya ndege nchini Iran tayari kuanza ziara na mazungumzo na viongozi wa serikali ya Iran jinsi ya kushirikiana kikamilifu kwa karibu sana. Korea ya Kaskazini yaonya mazoezi ya kijeshi ya pamoja.
Pyongyang, Korea ya Kaskazini - 27/11/2010. Serikali ya Korea ya Kaskazini imeonya kwa kusema ya kuwa "kitendo cha serikali ya Korea ya Kusini kufanya mazoezi ya kijeshi kwa pamoja na majeshi ya Amerika yanaweza kuleta tukio lisilo tabilika"
Hata hivyo serikali ya China imeitaka serikali ya Amerika kuangalia kwa makini kitendo chake cha kutaka kufanya mazoezi ya kijeshi pamoja na Korea ya Kusini.
China nchi ambayo inaushirikiano wa karibu na serikali ya imetuma ujumbe kwa serikali ya Korea ya Kusini ili kujadili swala hili.
Picha hapo juu zinaonekana ndege za kijeshi za Kiamerika zikiwa kwenye melikebu tayari kwa mazoezi.
Picha ya pili wanaonekana baadhi ya wananchi wa Korea ya Kusini wakiwa wamekusanyika mbele ya ofisi ya ulinzi kudai serikali ichukua hatua dhidi ya Korea ya Kaskazini.

No comments: