Thursday, May 24, 2012

Ugiriki yatakiwa kukamilisha matakwa ya nchi za Umoja wa Ulaya.

Rais wa zamani wa Tunisia huenda akahukumiwa adhabu ya kifo.



Tunisia, Tunis - 24/05/2012. Mwanasheria wa kijeshi ameiomba mahakama kumpa adhabu ya kifo aliyekuwa rais wa Tunisia aliyepinduliwa kutokana na maanamano ya wananchi mwaka 2011.
Mwanasheria huyo aliiomba mahakama kutoa adhabu kali ya kifo kwa  Ben Ali kwa  kusababisha mauaji ya watu 300 katika mji wa Kasserine, Tala, Kairouan na Tajrouine.
Zine al Abidine Beni Ali ambaye alikimbilia nchi Saud Arabia, January/14/2011 na kuachia madaraka, amesha hukumiwa kwenda jela, wakati hayupo nchini Tunisia kwa makoso ya kula rushwa na kutumia mali ya umma vibaya.
Ben Ali ambaye alitawala Tunisia kwa muda wa miaka 23 anashutumiwa kwa kuongoza nchi vibaya, kula rushwa na kuonea wanchi kwa kutumia  vyombo vya dola.

Ugiriki yatakiwa kukamilisha matakwa ya nchi za Umoja wa Ulaya.


Brussels, Ubeligiji - 24/05/2012. Viongozi wa nchi wanachama wa jumuiya ya Ulaya wamemaliza mkutano wao na kusisitiza ya kuwa Ugiriki lazima ikamilishe matakwa mkataba wa mabadiriko ya kiuchumi.
Rasi wa jumuiya ya Ulaya Herman Van Rompuy alisema " tunataka Ugiriki kubakia kuwa nchi mwanachama wa jumuiya ya Ulaya.
"Natunategemea ya kuwa baada ya uchaguzi nchi Ugiriki, serikali itakayo chaguliwa itafanya uamuzi bora ili iweze kusaidiwa kuinua uchumi wa nchi hiyo."
Mkutano huo wa viongozi wa nchi wanachama wa nchi za jumuiya ya Ulaya wamekutana ili kujadili hai halisi ya kiuchumi za nchi wanachama ili kuweka mkakati wa kujikwamua na myumbo wa uchumi uliopo kwa sasa.

Iran yatishia kujitoa katika mazungumzo na nchi za 5+1.

Baghdad, Irak - 24/05/2012. Serikali ya Iran imetishia kujitoa katika mazungumzo yanayo endelea kati yake na nchi za Marekani, Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, China na Urusi yanayo fanyika nchi Irak- Baghdad.
Kwa mujibu wa habari zinasema " nchi hizo tano ambazo ni wanchama wa kamati ya usalama ya umoja wa mataifa zimeshindwa kufikiana na matakwa ya Iran, kwani Iran inadai yakuwa mswada ulio pendekezwa hauna mabadiliko."
Hata hivyo Catherine Ashton waziri wa mambo ya kigeni wa jumuiya ya Ulaya aliongea na mwakilishi wa Iran katika majadiliano ya kinyuklia Saeed Jalili na Catherine Ashton alipo ulizwa nini kiliongelewa katika mkutano huo hakutoa jibu.
Mvutano kati ya Iran na  mradi wake wa kinyuklia na nchi za Ulaya Magharibi umepelekea Iran kuwekewa vikwazo na huku Iran ikidai yakuwa in haki ya kuendelea na mradi wake wa kinyuklia.

anchi wa Izrael wataka wakimbizi wa Kiafrika warudishwe kwao.

Tel-Aviv, Izrael - 24/05/2012. Maelfu ya wananchi nchi Izrael wamenadamana  kupinga kiterndo cha kuongezeka wakimbizi wa Kiafrika nchi humo.
Maandamano hayo ambayo yaliongozwa na  Michael Ben Ari ambaye ni mbuge kupitaia chama cha National  Union Part na Ben-Guir na Baruch Marzel ambao ni waandishi wa habari wenye msimamo mkali wa kisiasa wa upande wa kulia.
Waandamani hao walishika mabango yakupinga na kuilaumu serikali ya Benyamin Tetanyahu kwa kudai ya kuwa haifanyi lolote katika kuwaondoa wakimbizi nchini humo.
Izrael imekuwa na wakimbizi kutoka Sudan ya Kusini ambao wengi wao wameishi kwa muda mrefu nchini Izrael.

Ndege aina ya drone kutumika katika kuzuia ghasia.

Texas, Marekani - 24/05/2012. Polisi nchini Marekani wataweza kutumia ndege aina ya drone katika kutuliza ghasia.
Randy McDaniel ambaye ni mmoja wa  maafiasa wa polisi Texas alisema " hii itasaidia kuimarisha usalama hasa wakati wa vurugu."
Catherine Crump ambaye ni mfanayakazi wa American Civil Liberties Union alisema 2 halitakuwa jambo la busara ikiwa  ndege hizo zitaanza kutumika, kwani zinaweze leta madhara makubwa tofauti na polisi wa kawaida ambao huwa wapo katika matukio."
Ndege hizo aina ya drone zitakuwa na uwezo wa kubebe mabomu ya machozi na risasi zenye raba ambazo maranyingi utumika katika kuzuia ghasia.

Wednesday, May 23, 2012

Muuguzi aliye husika katika kifo cha Osama bin Laden afungwa jela miaka 33.

Urusi yazidi kujimarisha kiulinzi.


Moscow, Urusi - 23/-5/2012. Urusi imefanikiwa kurusha siraha ( bomu) linalo julikana kama intercontinental ballistic missile ambayo inauwezo wa kupambana na kubomoa siraha ya ina yoyote.
Habari kutoka wizara ya ulinzi ya Urusi zilisema " majaribio hayo yalifanyika kwenye eneo la Plesetsk."
Jaribio hilo la Urusi limekuja wakati Marekani inajadili mpango wa kuweka mitambo yake ya kiulinzi katika bara la Ulaya, jambo ambalo Urusi bado haijahafikiana na Marekani katika swala hilo.
Hata hivyo Marekani imekuwa ikisisitiza ya kuwa mitambo hiyo ya kiulinzi ni kwa ajili ya kuzilinda nchi wanacham wa NATO.

eshi la JM ya Kongo lapata wakati mgumu wa kulinda nchi.
Kinshasa, Jamuhuri ya Kidemokrasi Kongo - 23/05/2012. Jeshi la Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, limelaumiwa kwa kutotimiza kiapo cha kulinda wanchi kikamilifu.
Moja wa msemaji wa shirika linalo toa msaada kwa wakimbizi ( hakutoa jina) alisema " wanajeshi wa JM ya Kongo wanakuwa na wakati mgumu kutokana na kukusa mishahara na hata mishahara yenyewe ni midogo jambo jambo ambalo linawafanya kushindwa kutimiza swala la ulinzi wa raia na nchi.
"Vifaa vya kijeshi ambavyo wanatumia ni duni kulinganisha na vya kundi la upinzani linalo ongozwa na Bosco Ntaganda na wenzake ambao wanapingana na serikali ya Kinshasa inayongozwa na rais Joseph Kabila. 

Swala la Irani kuwa na nguvu za kinyuklia wa bado mvutano.

Baghdad, Iraq - 23/05/2012. Mkutano uliyo wakutanisha viongozi wa jumuiya ya kimataifa kutoka Ujerumani, China, Uingereza Urussi na Marekani wamekutana na viongozi wa Iran illikujadili kiundani kuhusu swala Iran kuwa na nyuklia.
Waziiri ambaye anashughurikia maswala ya nje ya nchi za jumjuiya ya Ulaya Catherine Ashton aliwakilisha muswada kwa viongozi wa Iran.
Hata hivyo shirika la habari la Iran IRNA limesema " muswada ambao umeletwa na Catherine Ashton hauna mageni na hauangalii faida za pande zote mbili na lazima ieleweke ya kuwa  pande zote mbili zifikie makubaliano ambayo yanafaida kwa nchi zote."
Iran imekuwa ikivutana na jumuiya ya kimataifa katika swala la haki ya nchi hiyo kuwa na uwezo wa nguvu za kinyuklia.

Muuguzi aliye husika katika kifo cha Osama bin Laden afungwa jela miaka 33.

Peshawar, Pakistan - 23/05/2012. Muuguzi ambaye alitoa uchunguzi wa kisayansi -DNA za aliyekuwa kiongozi mkuu wa kundi la Al Qaeda amehukumiwa kwend jela miaka 33.
Shakeel Afridi amakutwa na hatia ya kuhusika katika kufanya uhaini kwa kutoa habari za kisayansi ambazo nikinyume na sheria ya Pakistan
Mwezi January waziri wa ulinzi wa Marakani Leon Panetta alisibitisha kwa kusema " Afridi amekuwa mfanyakazi wa idara ya upelelezi ya Marekani CIA   kwa kutoa habari za kisayansi DNA ili kumjua na kumtambua aliyekuwa kiongozi wa kundi la Al Qaeda Osama bin Laden."
Shakeer Afridi alikuwa muuguzi wa kuheshimiwa na likamatwa wiki mbili baada ya kifo cha Osama bin Laden kufanywa na jeshi maalumu la Marekani.

Wamisri  wapiga kura  kumchagua rais wa nchi.

Kairo, Misri - 23/05/2012. Wananchi wa Misri wapiga kura leo ili kumchagua rais atakayeongoza nchi hiyo.
Uchaguzi huo wa rais wa Misri unafanyika kwa mara ya kwanza kushiriisha vyama vingi au uchaguzi wa kidemokrasia tangu kuangushwa kwa rais Husni Mubarak ambaye litawala Misri kwa miaka 30.
Viongozi wanaogombania uongozi wanatoka katika chama kinachojulikana Muslimu brothorhood, na viongozi ambao walikuwa wakati wa utawala wa rais Husni Mubarak.
Hamdy Abdel Salman ambaye ni mmoja ya mwakilishi wa Morsi alisme "  hadi kufikia sasa kila kitu kipo sawa japo kuwa watu walikuwa wanalalamika kuwepo kwa mistari mirefu."
Wanchi wa Misri anapiga kura  ili kupata kiongozi atakeye iongoza Misri kwa kufata misingi ya kidemokrasi baada ya miezi 15 kupita bila kuwa na serikali ya kudumu.

Monday, May 21, 2012

Ikulu ya Mali yavamiwa na rais ajeruhiwa vibaya na waandamanaji.

Waafghanistan kukabidhiwa ulinzi na usalama wa nchi yao na NATO 2014.

Chikago, Marekani - 21/05/2012.Viongozi wa nchi wanajumuiya wa nchi za  North Atlantic Treaty Organisation NATO, wamekubaliana kwa pamoja ya kuondoa majeshi ya NATO kuanzia 2013 nchi Afghanistan.
Viongozi hao ambao walikutana nchi Marekani Chikago, na kukubaliana ya kuwa uondokaji wa wanajeshi wa NATO utaanza taratibu naifikapo 2014 majeshi yote yatakuwa yamesha ondoka nchi Afghanistan.
Rais Baraka Obama ambaye alikuwa mwenyeji wa mkutano huo, alisema " nchi za jumuiya ya NATO 27  kuanzia mwaka 2014 swala la usalama wa Afghanistan litakuwa mikoni mwa jeshi Afghanistan, tutatoa misaada ya kimavunzo ili jeshi hilo liweze kuimarika vyema katika kulinda nchi ya Afghanistan."
Uamuzi huo wa viongozi wa wakuu wa NATO utafikisha kileleni vita vilivyo chukua miaka kumu katika kupambana chimbuko la ugaidi lililo kuwa na mizizi nchini Afghanistan. 

Ikulu ya Mali yavamiwa na rais ajeruhiwa vibaya na waandamanaji.

Bamako, Mali - 21/05/2012. Waandamanaji wamevamia Ikulu  ya rais wa  Mali na kumjeruhi vibaya rais wa mpito wa nchi hiyo.
Dioncounda Traore ambaye alikutwa na waandamanaji hao wakati akiwa ofisini na kupigwa hadi kupoteza fahamu na huku waandamanaji wakisema "hatukutaki kuwa rais na hatutaki matwakwa ya ECOWAS."
Msemaji wa hospitali aliyo lazwa rais huyo wa mali  Sekou Yuttara alisema "Dioncounda Traore aliletwa hapa hospitali akiwa hajitambuhi na ameumia vibaya." 
Diocounda Traore alichaguliwa kuongoza nchi katika kipindi cha mpito ili kuunda serikali baada ya makubaliano ya jeshi la Mali ambalo  jeshi lilifanya  mapinduzi ya kumng'oa madarakani rais  Amadou Toumani Toure wezi Machi 2012.

Mazishi ya aliyetumiwa kuangusha ndege ya Pan Am 103 yafanyika leo Trpol.

Tripol, Libya - 21/05/2012. Aliye kuwa mtuhumiwa na kukutwa na hatia  na mahakama ya kuingusha ndege ya Pan AM 103 amefanywa mazishi yake leo baada ya kufariki dunia jana.
Abdel Basset al Megrahi 60, alifariki duni kutokana na ugonjwa wa kansa ambao ulikuwa ukimsumbua kwa muda mrefu tangu akiwa gerezani nchini Scotland.
Abdle Nassar kaka wa marehemu Abdel Basset Megrahi alisema " hali ya ndugu yangu ilianza kuwa mbaya baaday ya kufanyika mapinduzi ya kuing'oa serikali ya Muammar Gaddafi, kwani dawa alizo kuwa nazo ziilibiwa baada ya kuvamiwa na hadi kifo cha Megrahi hakukuwa na mganga wa kumwangalia."
Watu wapatao 100 waliudhuria katika mazishi, na hapakuwepo na viongozi wa serikali ya mpito. 
Abdel Besset Megrahi alizaliwa mwaka 1952 na alisoma Marekani na kuishi Uingereza mapema miaka ya 1970.

Wakuu wa serikali ya Iran wakutana na Mkuu wa usimamizi wa maswala ya Kinyuklia duniani.

Tehran, Iran - 21/05/2012. Mkuu wa shirika linalo simamia maswala ya kiatomiki na nyuklia duniani International Atomic Energy Agency IAEA amewasili nchini Iran.
Yukiya Amano aliwasili nchini Iran na kufanya mazungumzo na mkuu wa maswala ya kinyuklia ya Iran Fereydoun Abbas Daveni.
Baada ya  mkutano huo Fereydoun Abbas Daveni alisema "tumefanya mazungumzo yenye uwazi ambao hauna kutiliana mashaka na kufanikisha maendeleo."
Yukiya Amano pia alikutana Saeed Jalili  msemaji mkuu wa maswala ya kinyukia ya Iran na waziri wa mambo ya nje  Ali Akbar Salehi.
Mkuu huyo wa shirika la kusimamia maswala ya kinyuklia ya kimataifa ametembelea Iran kabla ya mkutano utakao fanyika baghdad Irak kati ya Iran na wawakilishi wa jumuiya za kimataifa ili kujadili mpango mzima wa nyuklia ya Iran.

Sunday, May 20, 2012

Mshutumiwa wa mlipuko wa ndege ya Pan Am 103 afariki dunia.

Mshutumiwa wa mlipuko wa ndege ya Pan Am 103 afariki dunia.


Tripol, Libya - 20/05/2012. Raia wa  Libya ambaye alidai ya kuwa hakuwa na makosa ya kuhusika na mlipuko wa ndege ya shirika la Pan Am 103 mwaka 1988 amefariki dunia.
Abdelbeset Ali Mohmed al Megrahi 60, ye alikutwa na hatia na kuhukumiwa kwenda jela  miaka 27 kwa kosa la kuhusika katika ulipuaji wa ndege iliyo kuwa imebeba watu 270 ambapo watu wote walio kuwepo kwenye ndege hiyo walifariki dunia.
Abdulhakimu  ndugu wa  marehemu alisema " Abdelset A.M. Megrahi alifariki saa saba mchana 13:00 kwa saa za Libya."
Abdelbeset Ali Mohamed al Megrahi alihukumiwa kwenda jela mwaka 2001 nchini Scotland na baadaye aliachiwa huru   mwaka 2009 baada ya wauguzi kugundua ya kuwa alikuwa na ugonjwa wa kansa na kuruhusiwa kurudi nchini mwake Libya ambapo ilisadikiwa angeishi miezi mitatu, lakini aliweza kuishi miaka mitatu zaidi.

Vatikani yakumbwa na mtetemo wa uvumi wa habari.

Vatikan, Vatikn City - 20/05/2012. Papa Benedikt XVI ameteua  kamati maalumu ili kuchunguza kashfa za rushwa na matumizi  mabaya ya mzunguko wa pesa ambazo zimeenea hivi karibuni.
Kamati hiyo ambayo itashughulikia kiundani na kupata majibu ilikujua kama upo ukweli wa habari hizo.
Msemaji  wa Vatican Padri Federico Lombard alisema " kusambazwa ka habari hizo kumevunja sheria ya  na hipo haja kufuatilia ili sheria zichukuliwe."
Habari hizo pia  zina aminika kuelezea maisha ya binafsi ya Papa Benedikt VXI.

Mamia wapambana na polisi nchi Marekani.

Chicago, Marekani - 20/05/2012. Mamia ya watu waandamanaji katika jiji la Chicago wamepambana na polisi ambao walikuwa wanawazuia wasielekee kwenye eneo ambalo wakuu wa NATO wanafanya mkutana ili kujadili hali halisi ya shirikisho hilo.
 Kwa mujibu wa habari kutoka kwenye mkutano huo zinasema " moja ya swala muhimu ambalo litajadiliwa ni Afghanistan, "ambapo badhi ya nchi wanachama wa NATO wamesha tangaza kutoa majeshi yao nchini humo.
Katibu mkuu wa NATO Anders Fogh Rasmussen alisema " namatumaini ya kuwa swala la kuisaidia Afghanistan katika kulinda usalama wake litatiliwa mkazo na nchi za NATO, jambo ambalo litakuwa na faida kwa NATO na Waafghanistan."
Kwenye mkutano huo, rais wa Ufaransa Franois Hollande' atakuwa anaudhuria mkutano huo kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kuwa rais wa Ufaransa siku chache zilizo pita.

Chama cha Repabrikan cha Marekani chapitisha nguvu za kivita kwa Iran.

Washington, Marekani - 20/05/2012. Bunge la chama cha Republikan nchini Marekani limepiga kura na kupitisha muswaada wa kuishambulia Iran kama ikionekana usalama wa kinyuklia kwa Marekani.
Kura hizo zilizo pigwa 229 - 120 ambazo ziliunga mkono mswaadahuo.
Kwa mujibu wa katiba ya Mareakani katika maswala ya kiulinzi inasema " sheria  ya uamuzi wa ulinzi na usalama wa taifa itatumika kama ikihitajika katika kulinda usalama ikiwemo matumizi ya nguvu ya kijeshi."
Uamuzi wa bunge hilo umekuja wakati Marakani na Iran wanavutana katika mswala ya Iran kuwa na nyuklia.

Umoja wa Matifa waiwekea vikwazo Guinea Bissau.

New York, Marekani - 20/05/2012. Kamati ya usalama ya Umoja wa Matifa imeiwekea  vikwazo  serikali ya kijeshi Guinea Bissau baada ya kuchelewa kurudisha madaraka katika serikali ya kiraia.
Vikwazo hivyo ambavyo vimewekwa kwa viongozi wa kijeshi kutoweza kusafiri na kuhusishwa katika maswala ya kimataifa kama serikali.
Kamati hii iliamua kwa pamoja kwa kuiwekea Guinea Bissau  vikwazo vya kutoweza kununua siraha na matumizi ya aina yoyote ya kipesa.
Uamuzi huo umekuja kufuatia mapinduzi ya ambayo yamekuwa yakiikumba Guinea Bissau tangu mwaka 1974 tangu kupata uhuru kutoka kwa Wareno.

Saturday, May 19, 2012

Baraka Obama atanga mabilioni ya dola kwa kilimo barani Afrika.

Chelsea ya twaa ubingwa wa kombe la Ulaya kwa mara ya kwanza.

Munich, Ujerumani - 19/05/2012. Chelsea imechukua ubingwa wa kombe vilabu bingwa vya Ulaya kwa mara ya kwanza baada ya kuishinda timu ya Bayern Munich kwa penati 4-3 baada ya dakika 120 kumalizika kwa kila timu kufunga goli 1- 1.
Bayern Munich ilikuwa ya kwanza kupata goli lake kwa kupitia Tomas Muller katika dakika ya 83 na Didier Drogba alisawazisha katika dakika 88, jambo ambalo lilifanya mchezo huo kuisha 1-1 kwenye dakika 90 na baadaye mchezo huo kuendelea kwa kuongezwa dakika 30 za ziada ambapo zilikwisha  1-1 na mchezo huo kuamuliwa kwa penati na Chelsea kuchukua ubingwa wa kombe la Ulaya kwa msimu wa 2012-13.

 Wakuu wa nchi za G-8 wakubaliana Uguriki kubaki ndani ya jumuiya ya Ulaya.

Camp Davis, Marekani - 19/05/2012. Viongozi wa nchi za G-8 wamekutana nchini Marekani  na wamekubaliana kwa pamoja Ugiriki inatakiwa kubakia ndani ya jumuiya ya Ulaya.
Viongozi hao kutoka Marekani, Ujerumani, Japan, Uingereza, Urusi, Ufaransa, Canada na Itali walisema kwa pamoja " tunakubaliana kwa pamoja Greek ibaki katika jumuiya ya Ulaya wakati hali ya kiuchumi ya nchi hiyo kuwekwa sawa."
Viongozi hao ambao wapo nchini Marekani wamezungumzia pia maswala ya Korea ya Kaskazini na Iran, nchi ambazo zinavutana nazo katika maswala ya kinyuklia.

Mabomu nchini Syria yakutwa na mashaka ya kidemokrasia.

Deir az Zor, Syria - 19/05/2012. Mlipuko mkubwa ulitokea baada ya gari moja iliyokuwa imepakiwa mabomu kulipuka  karibu na maenao ya ofisi za usalama wa kijeshi.
Mlipuko huo ambao ulisababisha vifo vya watu wapatao  tisa na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa vibaya na kuharibu majengo pamoja na magari yaliyokuwa karibu.
Habari kutoka shirika la habari la serikali zilisema "mashambulizi hayo ni moja ya mbinu za wapinzani wa serikali wakisaidiwa na Al Qaeda."
Syria imekuwa ikikumbwa na milipuko ya mabomu tangu kuanza kwa mageuzi ya kidemokrasia amboyo yamekuwa yakileta misimamo tofauti kati ya serikali na wapinzani wake.

Rais Malawi kuingalia upya sheria ya kupinga ushoga.

 
Lilongwe, Malawi - 19/05/2012. Rais wa Malawi ametangaza yakuwa serikali yake itaiangalia upya sheria ya kupinga ushoga iliyopoyo pitishwa mwaka 1994.
Joyce Banda alisema baadhi ya sheria zilizopo  zinatakiwa kuangaliwa upya ikiwemo ile iliyo pitishwa kuhusu ushoga."
Pia rais Banda aliongezea kwa kusema " niwakati mgumu uliopo kwa serikali, kwani naogopa yakuwa kuwasili kwa rais wa Sudan Omar al Bashir  mwezi Julai kwenye mkutano wa nchi za Afrika kunaweza kuleta uhasama na nchi wahisani"
Rais Joyce Banda alichukua madaraka kufuatia kifo cha rais Mbingu wa Mutharika, na tangu kuingia madarakani nchi wahisani wameaanza kuendelea kutoa misaada, baada ya kuisimamisha kutokana na kupishana misimamo na nchi wahisani ikiwepo Uingereza.

Baraka Obama atanga mabilioni ya dola kwa kilimo barani Afrika. 

Washington, Marekani - 19/05/2012. Rais wa Marekani ametangaza yakuwa serikali ya Marekani itatoa kisa kikubwa cha pesa katika bara la Afrika ili kusaidia kilimo.
Baraka Obama " nijambo la kiiutu kusaidia bara la Afrika, a hakuna sababu kubwa inayo lifanya Afrika ishindwe kujilisha yenyewe.
"Serikali ya Marekani itatoa kiasi cha  dola za Kimalekani $3billion ambazo zitawezesha kuinua na kuimarisha kilimo bora na kuinua maisha ya wakazi wa Afrika."
Rais Baraka Obama, aliyatangaza hayo kabla ya kuanza kwa mkutano wa wakuu wa nchi G-8 ambao Obama atakuwa mwenyeji wa mkutano huo
Katika mkutano huo, viongozi wa nchi za Tanzania, Benin, Ghana na Ethiopia wamealikwa kushiriki katika mkutano huo.

Thabo Mbeki kujaribu kusuruhisha Wasudani.

Khartoun, Sudan - 19/05/2012.  Aliyekuwa rais wa Afrika ya Kusini amewasili nchini Sudan ili kujaribu kuleta usuruhishi wa kisiasa uliyopo kati ya Sudani Khartoum na Sudani ya Kusini.
Thabo Mbeki anatarajiwa kukutana na rais wa Sudan Omar al Bashir, wakati mapigano kati ya jeshi la Khartoum na Juba.
Sudan ya Kusini na Sudan - Khartoum zimekuwa zikivutana katika swala la mpaka ambao unazikutatisha nchi hizo mbili, ambapo inaaminika kwenye eneo hilo kuna malighafi za asili ambazo ni kiini cha uchumi wa kila upande wa nchi.

Wednesday, May 16, 2012

Charles Taylor adai mashahidi zidi yake walilipwa pesa

Charles Taylor adai walio toa ushahidi zidi yake walilipwa pesa.

Hague, Uhollanzi - 16/05/2012. Aliye kuwa rais wa Liberia na ambaye amekutwa na hatia ya kukiuka haki za binadamu na koti ya kutetea haki za binadamu amelaumu ya kuwa mashahidi walio kuja kutoa ushahidi zidi yake walipwa pesa.
Charles Taylor  64, alisema " Napenda kusema ya kuwa mashahidi walio kuja kutoa ushahidi zidi yangu walipewa pesa/kununuliwa na hata kutishiwa kushitakiwa ikiwa watakataa kuja kutoa ushahidi.
"Sikuwa na hatarisha maisha ya jamii kama inavyo daiwa, bali nilichokuwa najua ya kuwa ikiwa hakuna amani Sierra Leone, basi hata Liberia hakuta kuwa na amani.
"Mimi napinga na kulaani vitendo vyote vya kinyama, na ningependa uamuzi utakao tolewa na majiji uwe wa haki kuzingatia kiapo cha kazi zenu kwani mimi sasa ni mtu mzima na watoto naitwa babu. Vilevile ningependa kutoa masikitiko yangu kwa wale wote walio pata shida wakati wa vita. alisema Charles Taylor
"Japokuwa nipo hapa  inashangaza ya kuwa  viongozi wa nchi za Magharibi ambao wanauzia siraha makundi yanayo pigana kila sehemu na hasa bara la Afrika hakuna hata mmoja wao ambaye amesha wahi kushitakiwa au kushutumiwa kuhusika na vita na huu ndo ukweli wenyewe."
Wakili wa mahakama hiyo aliomba mahakama impe kifungo cha miaka 80 bwana Charlea Taylor
 wakati wa  kuhumu yake  mnomo tarehe 30 mwezi Mei 2012, atatumika kifungo chake nchi Uingereza kutokana  na makubaliano ya awali.
Hata hivyo mwana sheria anaye mwakilisha Charles Taylor alisema upo uwezekano wa kukata rufaa zidi ya adhabu ya kifungo itakapo tolewa.

Jeshi la Umoja wa Ulaya  la fanya mashambulizi nchi Somalia.

Haradhere, Somalia - 16/05/2012. Jeshi la nchi za jumuiya ya Ulaya limefanya mashambulizi kwa ndani ya Somalia kwa mara kwanza tangu kuanza ulinzi katika eneo hilo.
Jeshi hilo ambalo lilisafirishwa na helikopta hadi bandari Haradhere, ambayo inaamini kuwa kitovu cha maharamia ambao huvamia meli zinazo pita katika maeneo ya bahari  karibu na Somalia.
Bile Hussein ambaye ni msemajiwa wa  moja ya makundi ambayo yanashughurika na uharamia alisema " boti zao zenye mwendo wa kasi zilishambuliwa, pia baadhi ya maeneo yatu na vifaa vimeharibiwa vibaya na jeshi hilo la umoja wa Ulaya."
Serikali mpito ya Somalia   nayo ilithibitisha mashambyulizi hayo kwa kusema "mashambulizi hayo yalitokea kwa ushirikiano wa pamoja kati ya jeshi la Somalia na jeshi la umoja wa Ulaya."
maharamia waliopo nchi Somalia wamekuwa wakiziteka nyara meli zinazo pita katika maeneo yaliyopo karibu na bahari ya Somalia, nakusababisha hali ya uslama kuwa mashakani, jambo ambalo lili ifanya jumuiya ya kimataifa kuamua kuweka ulinzi katika maeneo hayo.

Serikali ya China ya chukuzwa na Serikali ya Uingereza.

Beijing, China - 16/05/2012.  Serikali ya China imelaani kitendo cha waziri mkuu wa Uingereza kukutana kiongozi wa kidini wa  Watibeti Dalai Lama.
Habari kutoka ofisi ya mambo ya nje ya China zilisema " kitendo hicho si cha busara na kinaingilia mambo ya ndani ya China na hakitaleta maantiki."
Nazo habari kutoka ofisi ya waziri mkuu wa Uingereza zinasema " waziri mkuu kukutana na Dalai Lama lilikuwa jambo muhimu, lakini wasingependa  swala hilo lilete kutoelewana kati ya China na Uingereza."
Dalai Lama ambaye alikimbia kutoka Tibeti 1959 na kufanya makazi yake Dharamsla India, baada ya jaribio la kutaka kuingausha serikali ya China kushindwa

Mji wa Mombasa wastushwa kwa mlipuko wa bomu.

Mombasa, Kenya - 16/05/2012. Wakazi wa mji wa  Mombasa nchini Kenya walistuliwa na mlipuko wa bomu uliotokea katika bar moja na kusababisha kifo cha mtu mmoja na wengine watano kujeruhiwa vibaya.
Mashambulizi hayo ya bomu yalitokea katika bar ya Bella Vista Club, baada ya watu wenye sirjha kuzuiliwa kuingia ndani na ndipo walipo rusha bomu ndani ya  bar hiyo.
Mkuu wa Polisi Mombasa Aggrey Adoli alismema " watu waliofanya mashambulizi, kwanza walianza kufyatua risasi na kumjeruhi mmoja wa walinzi na baadaye kurusha bomu."
Kenya imekuwa ikishambuliwa na mabomu kwa muda sasa  tangu jeshi la nchi hiyo kuingia nchini Somalia ili kupambana na kundi la Al Shabab ambalo linasadikiwa kushirikiana na kundi la Al Qaeda.

Tuesday, May 15, 2012

Francois Hollande aanza kazi yake urais rasmi leo nchi Ufaransa.

Francois Hollande aanza kazi yake urais rasmi leo nchi Ufaransa.

Paris, Ufaransa - 15/05/2012. Raia wa Ufaransa wapemepata rais mpya kutoka chama cha mrengo wa kushoto  cha Sosialisti tangu miaka 17 iliyo pita.
Francois Hollande ambaye alishinda uchaguzi wa rais hivi karibuni nchini Ufaransa aliapishwa rasmi leo kuwa rais wa Ufaransa baada ya Nicolas Sarkozy aliyekuwa rais kushindwa katika kura za kugombea kiti hicho cha urais wa Ufaransa kwa mara ya pili.
Rais Froncois Hollande alisema haya baada ya kuapishwa " ukurasa mpya umefunguliwa, ningependa kuwaapa huu ujumbe ya kuwa Wafaransa kuweni na imani, sisi ni taifa kubwa na huwa siku zote tuna pambana na kushinda magumu yanayo tukabili, na nahaidi ya kuwa  nitailinda na kuongoza kwa maadili bora ya ukweli, haki na usawa kwa kila Mfaransa."
Ushindi wa Francois Hollande umekuja baada ya kampeni yake kubwa ya kuhaidi kuleta mabadiliko ya kijamii na kiuchumi nchini Ufaransa kama akichaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo.


Luis Moreno Ocampo bado amsaka  Bosco Ntaganda na wenzake.

Hague, Uhollanzi - 15/05/2012. Mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za mauji na unyanyasaji wa haki za binadamu ipo mbioni kuhakikisha viongozi wa makundi ya kijeshi yaliyopo JD Kongo  wakamatwe.
Mwanasheria mkuu wa mahakama hiyo Luis Moreno Ocampo alisema " kuna baru ya kutaka Bosco Ntaganda na Sylvestre Mudacumura wakamatwe ili waje wajibu mashitaka ya kuhusika na ubakaji, unyanyasaji na mauji, watu hawa ni hatari saana."
Maoni hayo ya Ocampo yamekuja baada ya habari kupatikana ya mkuwa jeshi la umoja wa mataifa lilipo nchini JD ya Kongo kushambuliwa na na wanachi kwa madai jeshi hilo linashindwa kuwalinda kutokana na mashambulizi yanayo fanywa na makundi ya kijeshi yanayo pingana na serikali ya JD Kongo.
Viongozi hao wakijeshi waliopo nchini JD Kongo wamekuwa wanashutumiwa kwa kuhusika katika uchafuzi wa amani kwa kusababisha mauaji na ubakaji ambao uamekuwa yakitokea kwa muda mrefu sasa.


Muuaji wa mwanasayansi wa Iran anyongwa.


Tehran, Iran - 15/05/2012. Raia wa Iran aliyekutwa na hatia ya kumuua raia mwenzake ambaye alikuwa mwanasayansi wa mambo ya kinyuklia amenyongwa.
Habari kutoka shirika la habari la Iran zilisema "Majid Jamali Fashi ambaye alikutwa na hatia ya kumuua mwanasayansi  Profesa Massoud Ali Mohamed kwa kumtegea bomu mwaka 2010 alinyongwa hivi karibuni.
"Mtuhumiwa huyo ambaye pia alikutwa na hatia ya kuwa jasusi aliyetumiwa na idara ya upelelezi wa Izrael (MOSSAD) na inaamikiwa alipewa kiasi cha dola za Kimarekani $ 120,000 baada ya kukamilisha mauaji hayo."
Hata hivyo Izreal haikutoa maelezo yoyote kuhusu kuhusu huusiano uliopo kati ya Majid Jamali Fashi na MOSSAD kwa kusema "Izrael huwa aijadili au kuongelea maswala ya usalama kinyume na sheria."
Mauaji ya wanasayansi wanao shughuliklia maswala ya kinyuklia yameistusha serikali ya Iran na kutupia lawama  Marekani na Izrael kuwa ndizo nchi zinazo panga mipango ya mauaji ya wanasayansi wake.
Hata hivyo Marekani na Izrael zimekanusha kuhusika na mipango hiyo kwa kudai ni uzushi ambao usiyo na msingi.


Monday, May 14, 2012

Rais Hugo Chavez amaliza matibabu yake nchini Kuba

Rais Hugo Chavez amaliza matibabu yake nchini Kuba.

Karakas, Venezuela - 14/05/2012. Rais wa Venezuela ametangaza ya kuwa matibabu saratani (kansa)  aliyokuwa akifanyiwa nchini Kuba yamemalizika salama.
Rais Hugo Chavez 57 alisema" siku chache zilizo pita nilimaliza mzunguko wa matibabu yangu.
Nimekuja na matumaini makubwa yakuwa afya yangu itazidi kuwa nzuri na haya yote ni Mungu ana nitazidi kumwomba Mungu, siku zote tumwombe  Mungu atupe afya na uzima ili tuweze kumtumikia na kufanya kazi aliyo tuagiaza."
"Kwa baraka za Mungu na umwili wa askari ambao umeshughurikiwa na waganga kikamilifu, nitarudi  vitani mstari wa mbele katika kuendeleza mapinduzi ya kumomboa kila mwana Venezuela.
Nawashukuru wananchi wa wote wa Venezuela kwa maombi yenu na bila kuwasahahu wanachi wa Kuba chini ya Uongozi wa Raul Kastro na kaka yeke Fidel Kastro kwa kunipatia matibabu."
Hugo Chavez ambaye ametawala tangu 1999 amakuwa akienda nchi Kuba ili kufanyiwa matibabu ya kansa ambayo iligunduliwa na waganga wakati wa kuchunguza mwenendo wa afya yake.

Mmoja wa msaidizi wa Joseph Kony akamatwa.

Kampala, Uganda - 14/05/2012. Serikali ya Uganda imethibitisha kukamatwa kwa aliyekuwa mmoja ya viongoziwa kundi la Lord's Resistance Army (LRA) linalopingana na serikali ya Uganda.
Ceaser Achellam alikamatwa  nchi ya Afrika ya Kati kufuatia mipango ya kijeshi inayo endelea ya kutaka kuwakamata viongozi na wapiganaji wa LRA.
Msemaji wa jeshi la Uganda Felix Kulaigye alisema " kukamatwa kwa Achellema ni mafanikio makubwa kwani kutapunguza makali ya LRA, huyu Achelle ni mmoja wa samaki wakubwa wa LRA."
Serikali ya Uganda kwa msaada wa serikali ya Marekani zimekuwa zikimsaka kiongozi wa RLA Joseph Kony ambaye anadaiwa kuvuruga amani ya Waganda kwa muda wa miaka mingi sasa.

Umoja wa Mataifa wapitisha muswada wa kulinda ardhi za wenyeji.

New York, Marekani - 14/05/2012. Umoja wa Mataifa umekubali muswaada wa kihiyari  wa kusimamisha unyakuliwaji wa ardhi.
Muswaada huo ambao unazitaka serikali zote duniani, hasa zile zinazo tawala nchi masikini kusimamia haki za wanchi wao kikamilifu na kutouza au kukodisha ardhi hizo kwa makampuni ya kimataifa kwa kisingizio yanaleta maendeleo.
Maelezo yaliyo tolewa na  shirika la kimataifa la OXFARM yanaripoti ya kuwa kiasi cha heka million 200 zenye ukubwa wa Uingereza zimenunuliwa au kukodishwa na makampuni ya kimataifa katika nchi za Afrika na Asia."
Clara Jamart msemaji wa OXFARM alisema " kupitishwa kwa mswada huo ni mwanzo, kwani imechukua zaidi ya miaka mitatu ili kufanikisha muswada huu."
Kupitishwa kwa muswada huo kumekuja baada ya wasiwasi kuku ya kuwa makampuni ya kimataifa ya kutoka nchi tajiri yamekuwa yakitumia uwezo walionao kupata ardhi na hata kuwafanya wenye nchi kuwa na wakati mgumu kimakao hasa katika nchi za Ethiopia, Sudani ya Kusini, DR Kongo. 

NATO yaombwa kufanya uchunguzi vita vya Libya.

Gevena, Uswisi -14/o5/2012. Shirika linalo shughulikia na kusimamia haki za binadamu limetoa maelezo ya kuwa vita vilivyo ongozwa NATO ili kumng'oa Muammar Gaddafi vilisababisha mauji ya watu wasiyo na hatia.
Idara inayo simamia haki hizo ilisema " zaid ya watu 72 waliuwawa bila makosa kutokana na mashambulizi ya mabomu  ya anga yaliyofanywa na jeshi la NATO.
"Na NATO inabidi kufikilia swala kiuwajibikaji hilo kiundani zaidi."
Hata hivyo msemaji wa NATO Oana  Lungescu alisema " mashambulizi yote yaliyofanywa na NATO nchini Libya yalifuata sheria za kijeshi na yalifanywa katika maeneo yaliyo kuwa ya kijeshi, lakini katika hali ya kivita maisha ya watu huwa yanapotea kutokana na hali halisi.
"NATO ilifanya kila njia kuepuka kuleta maafa kwa raia na mali zao na kutoweka maisha yao hatarini."
Vita nchini Libya vilioongozwa na NATO kuwasaidia waliokuwa wanapinga serikali ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo Muammar Gaddafi ambaye uwawa katika mapinduzi hayo.

Tuesday, May 8, 2012

Vladmir Putin awa rais na Dmiry Medvedev awa waziri mkuu wake.

Vladmir Putin  awa rais na Dmiry Medvedev awa waziri mkuu wake.

Moscow, Urusi - 08/05/2012. Aliyekuwa waziri mkuu wa Urusi na kushinda uchaguzi wa urais nchini Urusi ameaanza kazi rasmi
Vladmir Putin ambaye amechaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo  kwa mara ya tatu, aliapishwa mbele ya wageni  2,000 waalikwa kushuhudia sherehe hiyo..
Putin ambaye  alichaguliwa hivi karibuni katika kinyang'anyiro cha kugombe urais wa Urusi amehaidi kuilinda na kuitete Urusi na watu wake kwa hali na mali.
Wakati huo huo aliyekuwa rais wa Urusi Dmitry Medvedev  amepitishwa na bunge la nchi hiyo  kuwa waziri mkuu wa Urusi  na anatarajiwa kuunda baraza la mawaziri  mara baada ya kula kiapo.


Hilary Clinton ushawishi kwa  India juu ya Iran  waleta mafanikio madogo


Newdelhi, India - 08/05/2012. Serikali ya India imepishana kimatakwa na serikali ya  Marekani kuhusu swala la ununuzi wa mafuta  kutoka Iran.
Waziri wa mambo ya nje wa India S.M Krishna alisema " tunafahamu umuhimu wa Iran kushiriki katika  mazungumzo ya  kinyuklia na vile vile  Iran ni  kiungo muhimu cha upatikanaji wa mafuta kwa India"
Waziri huyo wa mambo ya nje wa India aliyasema hayo, wakati alipo kutana na waziri wa mambo ya nje wa Marakani Hilary Clinton  ambaye yupo katika ziara ya kiserikali nchi India.

Makamu wa rais wa Irak atafutwa na polisi wa kimataifa.


Baghdad, Irak -08/05/2012. Serikali ya Irak imeliomba shirikisho la polisi dunia Interpol kumkamata aliyekuwa makamu wa rais wa nchi hiyo ambaye yupo mafichoni.
Kwa mujibu wa habari kutoka Interpol zinasema " aliyekuwa makamu wa rais wa Irak Tariq al Hashem
anatakiwa kukamatwa ili kujibu mashitaka ya kusaidia kifedha ugaidi."
Tariq al Hashem ambaye anatafutwa na serikali ya Irak kwa kudaiwa kuhusika na vitendo vya kiuaji alikimbia nje ya nchi baada ya kutokea kutokuelewana na serikali ya waziri mkuu wa Irak Nuri al Marik na kugomea kuingia bungeni kwa madai waziri mkuu huyo anatumia nguvu na kuhodhi madaraka yote.
Hata hivyo Tariq al Hashem amakuwa akikanusha madai hayo na kudai hizo ninjama za kisiasa na maisha yake yapo hatarini akirudi nchi Irak.

Sunday, May 6, 2012

Ufaransa yapata rais mpya Francois Hollande na Nikolas Sarkozy ashindwa uchaguzi.

Ufaransa yapata rais mpya Francois Hollande na Nikolas Sarkozy ashindwa uchaguzi.

Paris, Ufaransa - 06/04/2012. Matokeo ya uchaguzi nchini Ufaransa yamemng'oa madarakani  rais wa sasa wa nchi hiyo Nikolas Sarkozy.
Katika matokea ya uchaguzi huo aliyekuwa mpinzani wa  rais Sarkozy,  Hollande  ambaye anatarajiwa kuchukua ofisi ya urais pindipo atakapo apishwa alishinda kwa kupata asilimia 52% zidi ya Sarkozy 48%
Nikolas Sarkozy alisema " nimekubali kushindwa na watu wa Ufaransa wameongea kupitia kura zao."
Naye Francois Hollande ambaye ameshinda uchaguzi huo alisema " wananchi nawashurkuru kwa kunipa nafasi ya kuwa rais wa Ufaransa, na nitaifanya kwa moyo mmoja na kuilinda  Ufaransa na watu wote Waufaransa kuwa sawa na kupata haki sawa kuanzai mtoto hadi mkubwa.
"Ufaransa ni ya watu wote, kwani tumekuwa tukigawanywa na kuanzaia sasa ni mwisho na hakuna mtu ataruhusiwa kufanya hivyo na niwajibu wangu kutimiza ya kuwa kila Mfaransa lazima ashirki katika kujenga taifa letu na lazima tuaandae taifa la vijana wa kesho wa Kifaransa na sisi ni Wafaransa na lazima tujue hili.
"Amani, usawa na haki za binadamu na kila ambacho kinahitajika kwa binadamu lazima kila Mfaransa  apate viva Ufaransa."
Matokeo ya uchaguzi nchini Ufaransa nchini Ufaransa yalikuwa yanatazamiwa tangu hapo mwanzo yalikuwa 
ya vuta ni kute kati ya Sarkozy na Hollende kutokana na  kupishana kimirengo ya kisiasa.

Mamia waandamana kupinga kuapishwa kwa Vladmir Putin.

Moscow, Urusi - 06/05/2012. Baadhi ya mamia ya watu wameandaman jiji Moscow ili kupinga kitendo cha kutaka kuapishwa kwa rais Vladimir Putin.
Kufuatia maaandamano hayo watu wapatao 400 wamekamatwa na polisi kwa kufanya vurugu kinyume na sheria.
Habari kutoka kwa msemaji wa polisi zinasema " watu 20,000 wameudhuria katika maandamano hayo.
Waandamanaji hao walikuwa wamebeba mabango yaliyo andikwa " tumechokwa kudanganywa."
Tangu kuchaguliwa kwa  Vladimir Putin kuwa rais,  Urusi imekuwa ikikumbwa na maandamano ya hapa na pale kwa kupinga kitecho hicho cha kuchaguliwa kwake kuwa rais.

Baraka Obama aanza kampeni za uchaguzi rasmi.


Columbus, Marekani - 06/05/2012. Rais wa Marekani ameanza kampeni ya urais nchini humo ambao unatazamiwa kufanyika mwaka huu.
Baraka Obama alisema " Demokrati watashinda uchaguzi kwa kutumia mikakati yake ile ile ya kuwahusisha wananchi kwa kuwatembelea mlango kwa mlango mtaa kwa mtaa ili kuwahakikishia  Wamarekani ya kuwa bado wanauwezo wa kungoza nchi.
" Lazima tukumbuke ya kuwa tunasonga mbele na haturudi nyuma."
Rais Baraka Obama anatarajiwa na kugombania urais na mpinzania wake wa chama cha Republikani  Mitt Romney ambaye amehaidi pia kuwa atamshinda Baraka Obama.


Wasudani wakubaliana na mpango wa Umoja wa Afrika.


Adis Ababa, Ethiopia - 06/05/2012. Mpango wa kuleta amani nchini Sudan ambao ulipendekezwa na  umoja wa nchi za Africa ili kuleta amani ubekubalika.
Sudan na Sudai ya Kusini zimekubaliana kutimiza mpango wa kuleta amani  kawati ya nchi hizo mbili ambao ulipendekezwa  ili kuhakikisha yakuwa amani inakuwepo.
Mpango huo wa kuwepo wa kuwa mbinu  saba ambao utazikutanisha nchi hizo mbili katika meza ili kujadili ni kwa jinsi gani amani itakuwepo kati yao.

Thursday, May 3, 2012

Mtoto wa Muammar Gaddafi ataka Luis Moreno Ocampo kuchunguza kifo cha baba yake.

Urusi ya toa taadhari kwa ikiwa mitambo ya kijeshi itawekwa barani Ulaya na Marekani.


Moscow, Urusi - 03/05/2012. Serikali ya Urusi imesisitiza ya kuwa  inauwezo wakutumia nguvu zake za kijeshi na kushambulia mitambo ya kijeshi ya Marekani itakayo wekwa Ulaya.
Chief Generali Staff Nikolay Makarov alisema " ikiwa mitambo ya ABM ya Marekani itawekwa bila kufikia makubaliano na kusababisha hali ya usalama wa Urusi kuwa katika hali isiyo ridhisha, basi hakuna njia nyingine ni kuizuia kwa kutumia mbinu za kijeshi.
" Urusi haina mipango wa kuweka mitambo yake ya kivita nje ya nchi."
Mvutano kati ya Urusi na Marekani kuhusu kuwekwa kwa mitambo ya kijeshi ya Marekani barani Ulaya kwa madai yakuwa ni kwaajili ya kulinda usalama wa Marekani na washiriki wake zidi Iran, jambo ambalo Urusi inalitilia mashaka ya kuwa ni mmpango wa Marekani wa kutaka kukuza uwezo wa kijeshi barani Ulaya. 

Mtoto wa Muammar Gaddafi ataka Luis Moreno Ocampo kuchunguza kifo cha baba yake.

Algeirs, Algeria - 03/05/2012.  Mtoto wa kike  wa aliyekuwa rais wa Libya amemwandikia mwanasheria mkuu wa mahakama ya kimataifa kwa kutaka kesi ya ukiukwaji wa haki za binadamu ifunguliwe ili kuchunguza chanzo cha kifo cha baba yake mzazi.
Aisha Gaddafi ambaye yupo makimbiloni nchini Algeria alisema kupitia mwanasheria wake Nick Kaufman " ningependa kuchukua nafasi hii kuwakumbusha makubaliano ya Rome ambayo ndiyo msingi mkubwa wa Mahakama ya kiamtaifa inayaoshughulikia utetezi wa haki za binadamu  na naomba mwanasheria wa mahama hiyo  afanye uchunguzi wa kifo cha baba yangu Muammar Gaddafi na kufikisha swala hili kwa kamati ya usalama ya umoja wa mataifa."
Aisha Gaddafi ambaye pia ni mwanasheria amekuwa akisimamia swala la kutaka kufanyika uchunguzi wa kifo cha baba yake ambaye aliwawa baada baaada ya serikali yake kuangushwa na kundi la wapinzani kwa msaada wa NATO.

Serikali ya Marekani yatoa siri na mipango ya Osama bin Laden.

Washington, Marekani - 03/05/2012. Serikali ya Marekani imechapisha kwenye mitandao baadhi ya maelezo na mipango ambayo ilikuwa imeandaliwa na kiongozi wa kundi la Al Qaeda.
Maelezo hayo na mipango hiyo imechapishwa kwenye mtandao wa idara inayo simamia maswala kupigana na ugaidi Combating Terrorism Centre ikiwa ni moja ya  kurasa za maelezo 6,000 ambazo zilipatikana baada ya kumvamia kiongozi wa kundi hilo la Al Qaeda Osama bin Laden mwaka jana May 2011 nchi Pakistan na kumua.
Kwa mujibu wa habari zilizo patikana zinasema " maelezo yalipatikana kwenye faili za mitandao ya mtandao aliyokuwa akitumia Osama bin Laden."
Wakati huo huo baadhi ya wananchi wameendamani nchi Afghanistan katika kuadhimisha mwaka mmoja tangu kuuwawa kwa kiongozi wa kundi la Al Qaeda na jeshi la  Mareakani mwaka 2011 may.
Kutolewa kwa maelezo hayo kumekuja siku mbili baada ya  rais wa Marekani baraka Obama kumaliza kufanya ziara nchi Afghanistani na kusisitiza ya kuwa jeshi la Marekani litakabidhi maswala ya ulinzi wa Afghanistan kwa jeshi la nchi hiyo muda si mrefu.