Tuesday, May 8, 2012

Vladmir Putin awa rais na Dmiry Medvedev awa waziri mkuu wake.

Vladmir Putin  awa rais na Dmiry Medvedev awa waziri mkuu wake.

Moscow, Urusi - 08/05/2012. Aliyekuwa waziri mkuu wa Urusi na kushinda uchaguzi wa urais nchini Urusi ameaanza kazi rasmi
Vladmir Putin ambaye amechaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo  kwa mara ya tatu, aliapishwa mbele ya wageni  2,000 waalikwa kushuhudia sherehe hiyo..
Putin ambaye  alichaguliwa hivi karibuni katika kinyang'anyiro cha kugombe urais wa Urusi amehaidi kuilinda na kuitete Urusi na watu wake kwa hali na mali.
Wakati huo huo aliyekuwa rais wa Urusi Dmitry Medvedev  amepitishwa na bunge la nchi hiyo  kuwa waziri mkuu wa Urusi  na anatarajiwa kuunda baraza la mawaziri  mara baada ya kula kiapo.


Hilary Clinton ushawishi kwa  India juu ya Iran  waleta mafanikio madogo


Newdelhi, India - 08/05/2012. Serikali ya India imepishana kimatakwa na serikali ya  Marekani kuhusu swala la ununuzi wa mafuta  kutoka Iran.
Waziri wa mambo ya nje wa India S.M Krishna alisema " tunafahamu umuhimu wa Iran kushiriki katika  mazungumzo ya  kinyuklia na vile vile  Iran ni  kiungo muhimu cha upatikanaji wa mafuta kwa India"
Waziri huyo wa mambo ya nje wa India aliyasema hayo, wakati alipo kutana na waziri wa mambo ya nje wa Marakani Hilary Clinton  ambaye yupo katika ziara ya kiserikali nchi India.

Makamu wa rais wa Irak atafutwa na polisi wa kimataifa.


Baghdad, Irak -08/05/2012. Serikali ya Irak imeliomba shirikisho la polisi dunia Interpol kumkamata aliyekuwa makamu wa rais wa nchi hiyo ambaye yupo mafichoni.
Kwa mujibu wa habari kutoka Interpol zinasema " aliyekuwa makamu wa rais wa Irak Tariq al Hashem
anatakiwa kukamatwa ili kujibu mashitaka ya kusaidia kifedha ugaidi."
Tariq al Hashem ambaye anatafutwa na serikali ya Irak kwa kudaiwa kuhusika na vitendo vya kiuaji alikimbia nje ya nchi baada ya kutokea kutokuelewana na serikali ya waziri mkuu wa Irak Nuri al Marik na kugomea kuingia bungeni kwa madai waziri mkuu huyo anatumia nguvu na kuhodhi madaraka yote.
Hata hivyo Tariq al Hashem amakuwa akikanusha madai hayo na kudai hizo ninjama za kisiasa na maisha yake yapo hatarini akirudi nchi Irak.

No comments: