Thursday, July 9, 2009

Majina ya walioanzisha vurugu nchini Kenya yakabidhiwa kwa ICC.

Mgomo waleta kichwa kuuma kwa wapenzi wa soka duniani.

Cape Town, Afrika ya Kusini - 09/07/09. Maelfu ya wafanyakazi wanaofanya kazi katika ujenzi wa viwanja vya mpira wa miguu, ambavyo vitatumika katika kuchezea fainali za mpira wa miguu za kombe la dunia 2010 nchini Afrika ya Kusini, wameanza mgomo wao leo, kwa kudai waongezwe malipo ya kipato chao (mshahara) kufikia (asilimia) 13%.
Akiongea na waandishi wa habari, mmoja ya wafanyakazi wa viwanja hivyo 10 vya mpira wa miguu,Martin Baloyi, alisema hayo huku akiwa amelala katika vyuma vya kujengea,yakuwa wanataka wapate pesa ambazo ni haki kwao.
Kwa kipindi cha miezi miwili sasa vyama vya wafanyakazi viwili na South Africa Federation of Civil Engineering Contractors, vimekuwa katika majadiliano bila kufukia muafaka. Vyama hivyo vinavyo wakilisha wafanyakzi wapatao 70,000,, vimedai yakuwa wafanyakazi wamekuwa wakipata malipo ya $ 1.75, kwa saa na vyama hivyo vinataka kipato hichao lazima kiongezwe.
Kufuatia mgomo huu, hali ya ukamilishwaji wa viwanja hivyo kwa ajiliya mshindao hayo, huenda ukaleta kichwa kuuma kwa serikali ya Afrika ya Kusini.
Picha ya kwanza, wanaonekana wafanyakazi wa ujenziwa moja ya kiwanja jijini Cape Town, wakiandamana kudai kipato kiongezeke.
Picha ya pili juu, wanaonekana baadhi ya wafanyakazi wa kujenga moja ya kiwanja cha mpira wakiwa wamekaa chini baada ya kuanza mgomo,huku nyuma yao ni kiwanja cha mpira wa miguu kikiwa hakijakamilika ujenzi wake.
Majina ya lioanzisha vurugu nchini Kenya, yakabidhiwa kwa ICC.
Hague, Uhollanzi - 09/07/09. Katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan, amekabidhi majina ya watu waliohusika katika vurugu wakati na baada ya uchaguzi wa Kenya, uliofanyika mwaka 2007.
Kwa mujibu wa habari, zinasema Kofi Annan, alimkabidhi mwanasheria wa mahakama inayo shughulikia makosa ya ukiukwaji wa haki za binadamu, bwana, Moreno Ocampo.
Hata hivyo, swala hilo halikuwafurahisha baadhi ya viongozi wa Kenya, kwani walikuwa wanadai yakuwa kesi za watu hao ingebidi zisikilizwe nchini Kenya, lakini baadhi ya viongozi wengine walisema,ikiwa kesi hizo sitasikilizwa nchi Kenya, huenda kukakiukwa baadhi ya sheria na kutakuwa hakuna njia bora ya kuwalinda mashahidi.
Hapo juu,anaonekna Kofi Annan, akiwa amefunga mkono, huku akiangali juu.
G8, zahaidi kushirikiana kupunguza uzalishaji wa hewa chafu duniani.
Laquila, Itali - 09/07/09. Viongozi wa nchi tajiri duniani, G8 wanaendelea kukutana nchini Itali, kujadili ni jinsi gani, zitashirikiana kupunguza uzalishaji wa hewa chafu inayozalishwa na viwanda vikubwa, mitambo mikubwa na teknoloji zinazo atarisha mazingira na viumbe vyake kwa ujumla.
Wakiongea kwa nyakati tofauti, wakiongozwa na rais, Baraka Obama, walihaidi kupunguza hewa chafu kwa kiasi cha (digree) nyuzi 2 celsius mpaka itakapo fika 2050.
Akiongea kusisitiza hayo rais Amerika , Baraka Obama, alisema ya kuwa viongozi wa sasa wana deni kubwa ambalo itawabidi washirikiane ili kulinda hali ya hewa isichafuliwe zaidi na hewa chafu inayo tokana kukua kwa maendeleo ya nchi tajiri, na akashauri ni lazima nchi tajiri ziangalie na kubuni mbinu mpya za kuleta maendeleo bila kuharibu mazingira kwani hakuna wa kulaumiwa, hili ni jukumu la kila nchi na watu wake.
Picha hapo juu wanaonekana viongozi wa G8, wakiwa pamoja baada ya mkutano wao kwanza kuisha.
Hali ya usalama wa Irak,bado mthiani kwa serikali ya Irak.
Tal Afar,Iraq - 09/07/09.Watu wapatao 33wamefariki dunia kwa mlipuko wa mabomu, baada ya mauaji ya kujitolea muhanga kulipuka sehemu tofauti, na kuacha zaidi ya watu 70, wamejeruhiwa vibaya.
Kwa mujibu , wa msemaji wa polisi,Kanali, Khaled Omar, mashambulizi hayo, yametoke karibu na ofisi za mahakama.
Wakati huo huo, kwa mujibu wa habari zilizotolewa na serikali, zina sema zaidi ya watu 437, wamepoteza maisha tangu kutangazwa kwa jeshi la Amerika, kulipa madaraka jeshi la Iraq.
Picha hapo juu, anaonekana kijana, mmoja ambaye ameumia vibaya baada ya kuwa katika eneo bomu lililolipuka.

No comments: