Sunday, July 12, 2009

Rais wa Amerika , Baraka Obama, Barani Afrika.

Rais , Baraka Obama, awasili barani Afrika kwa mara ya kwanza akiwa rais wa Amerika.

Akkra Ghana - 11/07/09 . Rais wa Amerika, Baraka Obama, amefanya ziara ya siku moja ya kiserikali nchini Ghana, ikiwa ni kuonyesha ya kuwa serikali yale inatilia mkazo uhusiano Amerika na Afrika.
Katika ziara hiyo, rais Obama, alisema viongozi wa Afrika, wana jukumu kubwa la kujenga na kuendeleza nchi zao kwa misingi uongozi bora kwani wa Afrika ndiyo watakao jenga Afrika.
Picha hapo juu, anaonekana, rais Baraka Obama, akipokea heshima kutoka kwa jeshi la Ghana, kabla ya kuanza rasmi mazungumzo na viongozi wa serikali ya Ghana.
Picha ya pili,anaonekana, rais Baraka Obama, akiongoea mara baada ya kuwasili nchini Ghana.
Picha ya tatu, rais Baraka Obama, mtoto wake Sasha na mtunza jumba la Cape Coast Castle, akiwapa maelezo kwa undani jinsi gani watumwa walivyo kuwa wakitolewa katika jumba la Cape Coast Castle, na kupitia kwenye mlango ambao wanatokea, mlango ambao watumwa alikuwa wakitolewa tayari kwa kusafirishwa kwenda Amerika na kwingine duniani, kuwa watumwa.
Picha ya nne, anaonekana , rais Baraka Obama, akiwa na mwenyeji wake, rais wa Ghana, John Atta Mills, wakielekea kwenye ofisi za Ikulu ya Ghana, tayari kwa mazungumzo.
Picha ya pili, anaonekana, rais Baraka Obama, akiongea na viongozi na wananchi wa Ghana.
Picha ya tano wanaonekana, rais Baraka Omba na mke wake, Michelle Obama, wakiwa waslimia wauguzi na wagonjwa wa hospitali kuu ya jijini Akkra.

No comments: