Monday, July 6, 2009

Urussi na Amerika zakubaliana kushirikiana katika swala la nyuklia. Moscow, Urussi - 06/07/09. Urussi na Amerika zimekubaliana kupunguza siraha za nyuklia, wakati marais wa nchi hizo walipo kutana leo siku ya jumatatu jijini Moscow. Makubaliano hayo,yamefanyika wakat Rais wa Amerika , baraka Obama, akiwa ziarani Urussi, kuongea na viongozi wa Urussi,ili kudumisha uhusiano, ambao ulikuwa umeingia utata, baada ya Amerika kutaka kuweka makombo yake katikati mwa Ulaya, kwa kudai ni kaajili ya kulinda mashambulizi ambayo yanaweza kutokea Iran au Korea ya Kaskazini, lakini Urussi ilililikataa jambo hilo na likazusha mgogoro. Picha hapo juu, wanaonekana rais wa Amerika, Baraka.H.OBama, akiongea na rais wa Urussi Dmitri . A. Medvedev wakati walipo kutana kwa mazunguzo ya kikazi jijini Moscow.

No comments: