Muungano wa Ulaya wapata rais mpya. Brussels, Ubeligiji - 14/07/09.Mbuge wa Poland, Jerzy Buzek, amechaguliwa kuwa rais wa bunge la muungano wa Ulaya, baada ya kuchaguliwa kwa kura nyingi zaid ya 555 kati ya kura 644 zilizo pigwa katika uchaguzi wa rais wa bunge la muungano wa Ulaya. Mbunge, Jerzy Buzek, ambaye ni mbuge wa mlango wa kati kimsimamo, amechaguliwa, ikiwa nchi yake ina miaka minne tangu kujiunga na muungano wa Ulaya. Picha hapo juu, anaonekana, rais wa sasa wa muungano wa Ulaya, akiongea mara baada ya kuchaguliwa kwake.
Hague, Holland - 14/07/09. Rais wa zamani wa Liberia, Charles Taylor ametoa ushahidi wake leo zidi ya makosa 11, ambayo yanamkabili.
Akiongea, mbele ya jaji, rais huyo wa zamani wa Liberia,Charles Taylor,alisema ya kuwa makosa zidi yake ni ya , uzushi,uongo ulio jaa fununu za ajabu,uvumi, na hayana ukweli ndani yake na wale wanao zania ya kuwa yeye alihusika,katika mauaji na machafuko ya liyotokea nchini Sierra Leone.
Machafuko na mauaji hayo yaliyo tokea mwaka 1991 - 2001, yalipoteza maisha ya watu wapatao 200,000. Hata hivyo kesi hii bado inaendelea. Picha hapo juu, anaonekana, rais wa zamani wa Liberia Charles Tayrol kushoto, akiwa mahakamani kutoa ushahidi wake.
No comments:
Post a Comment