Sunday, December 5, 2010

Umoja wa Afrika watuma mjumbe kuleta suruhu za kisiasa nchini Ivory Coast

Umoja wa Afrika watuma mjumbe kuleta suruhu za kisiasa nchini Ivory Coast. Abidjan,Ivory Coast - 05/12/2010. Rais wa pili wa Afrika ya Kusini tangu kushindwa kwa utawala wa kibaguzi wa rangi, Thabo Mbeki amewasili jijini Abidjan ili kuleta suruhisho la matokeo ya uchaguzi wa rais. Kwa mujibu wa habari zilizo patikana zinasema "Thabo Mbeki ameteuliwa na Umoja wa Afrika (UA) kushughulikia swala la matokeo ya uchaguzi wa Ivory Coast, ambapo rais mtetezi Laurent Gbagbo waliapishwa kuwa rais, ingawaje apo awali kamati ya uchaguzi ilimtangaza mpizani wake Allasane Ouattara kuwa mshindi kwa kupata kura nyingi zaidi." Kuwasili huko kwa Thabo Mbeki kunatarajiwa kuleta suruhisho ili kuepuka mvutano wa kisiasa. Uchaguzi nchini Ivory Coast uliwahi kuhairishwa zaidi ya mara tano kutokana na mvutano wa kisiasa. Picha hapo juu ni ya aliyekuwa rais wa Afrika ya Kusini Thabo mbeki, ambaye anatarajiwa kuleta suruhisho la kisiasa nchini Ivory Coast.

Jeshi la Umoja wa Afrika kuwa na wakati mgumu.
Mogadishu, Somalia - 05/12/2010. Kundi la Al-Shabab lililopo nchini Somalia limesema litaendelea kupambana na majeshi ya wageni waliovamia nchi yao.
Maelezo hayo yalitolewa na mmoja wa kiongozi wa wapiganaji kwa kusema " wamevamia nchi yetu na hatuna budu kuitetea."
Kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za binadamu zinasema "zaidi ya watu mia moja wamefariki katika kipindi cha miaka mitatu tangu kuanza mapambano kati ya Al-Shabab na jeshi la UA ."
Picha hpo juu wanaonekana wanajeshi wa Umoja wa Afika wakiwa katika mazoezi ya kijeshi ili kupambana na kundi la Al-shabab.
Picha ya pili ni ya kundi la Al-Shabab kundi ambalo limekuwa ilikiendeleza mashambulizi zidi ya wanajeshi wa umoja wa Afrika na raia ambao wanakwenda kinyume na Al-Shabab.
Iran yatangaza kuzalisha madini ya kinyuklia.
Tehran, Iran 05/12/2010. Serikali ya Iran imetangaza ya kuwa wanasanyansi wake wameweza kuzalisha kwa mara ya kwanza madini ya ambayo yanatumika katika kuzalisha nguvu za nyuklia.
Akiongea mkuu huyo wa maswala ya kinyuklia Ali Akbar Salehi alisema "Iran itaanza kutumia madini yake hayo kwa mara ya kwanza ambayo yamezalishwa hapa nyumbani na kutotegemea kuagiza toka nchi za nje."
Kitendo cha Iran kutangaza uwezo wake huo, kutazidi kuleta vichwa kuuma kwa Amerika na nchi nyingine ambazo haziamini ya kuwa Iran haina mpamgo wa kutengeneza siraha za kinyuklia.
Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya wanasayansi wa Irani wakiwa kazini katika kiwanda cha kuzalishia nguvu za kinyukli.
Wamisri wapiga kura tena kuwachagua viongozi wao.
Kairo,Misri - 05/12/2010. Wanachi wa Misri wamepiga kura kwa mara ya pili ili kuwachagua wabunge.
Uchaguzi huo wa mara ya pili wa kuchagua wabunge unafanyika huku vyama vya upinzani vikiwa vimejitoa kwa kupinga ya kuwa uchaguzi huo si harali.
Uchaguzi huo ambao chama tawala (NDP)-National Democratic Party) kinatarajiwa kushinda viti vingi kutokana na kujitoa kwa vyama vya upinzani.
Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya wadau wa vyama vya upinzani wakiwa wametawanywa na polisi wa kuzuia ghasia wakati wa maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa awali.

No comments: