Tuesday, December 7, 2010

Urussi kuwa mwanachama wa World Trade Organazations

Mwanzilishi wa mtandao wa Wiki Leaks awekwa kizuizini

London, Uingereza -07/12/2010. Mahakama ya jijini London imemkatalia dhamana mwanzilishi wa mtandao wa Wiki Leaks ambaye alijipeleka mwenyewe polisi.
Julian Assange 39, aliwasili kwenye kituo cha polisi na baadaye kufikishwa mahakamani kutokana na kesi ya kufanya mapenzi ya kushutukiza iliyofunguliwa juu yake nchni Sweden.
Mwanasheria wa serikali wa Sweden aliomba mahaka kutompa dhamana Julian Assange kwa kuwa hajulikani anapoishi."
Hata hivyo mwanasheria Mark Stephens,ambaye anamwakilisha Julian Assange alisema " tutakata rufaa siku ya Jumanne wiki ijayo na ikiwezekana tutaenda mahamaka kuu na nina amini ya kuwa mahakama ya Uingereza itataua swala hili bila matatizo. "
Picha hapo juu ni ya Julian Assange ambaye mtandao wake umetikisa ulimwengu wa siasa na wa kidiplomasia baada ya kuchapisha habari za siri.
Waziri mkuu wa Uingereza afanya ziara ya ghafla nchini Afghanistan.
Kabul, Afghanistan - 07/12/2010. Waziri mkuu wa Uingereza amefanya ziara ya ghafla nchini Afghanistan na kukutana na rais wa nchi hiyo.
Waziri mkuu David Cameron, aliongea mbele ya waandishi wa habari alisema " uhusiano wa wanchi wa Afghanistani na Uingereza utazidi kudumishwa na jumuiya ya kimataifa ishirikiane kuijenge Afghanistan."
Hata hivyo David Cameron, aliongezea kwa kusema " natumaiini hali itazidi kuwa nzuri na itaturuhusi kuanza kufikiria kuondoa majeshi yetu ifikikapo mwakani."
Kabla ya kuongea na rais Hamid Karzai, David Cameron alitembelea wanajeshi wa Uingereza waliopo katika jimbo la Helmond.
Picha hapo juu anaonekana waziri mkuu wa Uingereza David Cameron kushoto akiwa na mwenyeji wake rais wa Afghanistan Hamid Karzai kulia wakati walipo kuwa wakiongea na waandishi wa habari.
Urussi kuwa mwanachama wa World Trade Organazations 2011.
Brussels, Ubelgiji - 07/12/2010. Jumuiya ya Ulaya imekubali na kuunga mkono kwa Urussi kuwa nchi mwana chama World Trade Organizatio, (WTO) ifikapo mwaka 2011.
John Clancy mbaye ni msemaji wa jumuiya ya Ulaya alisema "tumetia sahihi mkataba huo na Urussi baada ya kufikia maafikiano kwa pamoja."
Kukubaliwa huko kwaUrussi kuwa mwanachama wa WTO kutainua kwa kiasi kikubwa uchumi kati ya nchi wanachama na inakakadiliwa kufika kiasi cha asilimia 3.3 na hata kuongezeka katika siku za mbele.
Picha hapo juu wanaonekana viongozi wa Urussi na jumuiya ya nchi za Ulaya wakiwa katika mkutano ili kujadili nini cha kufanya ili kudumisha uhusiano wa karibu.
Mazungumzo ya kinyuklia na Iran bado kitendawili.
Geneva,Uswis - 07/12/2010.Mkutano wa mazungumzo kati ya Iran na nchi za jumuia ya Ulaya, nchi wanachama wa kudumu wa kamati ya usalama ya umoja wa Mataifa
Urussia,China,France, Uingereza, Ujerumani na Amerika umekwisha bila lengo la mkutano huo kufikiwa.
Saeed Jalili ambaye ni mkuuwa wa maswala ya kinyuklia ya Iran,alisema "hatutazungumzia maswala ya maendeleo yetu ya kinyuklia na uzalishaji wake katika kikao kijacho amabcho kinatarajiwa kufanyika Instambul nchini Uturuki na kuhusu swala hilo basi lazima kuwepo na ushirikiano kutoka pande zote mbili."
Naye mmoja wa wajumbe toka Amerika alisema "matarajio ya mkutano wetu hayakufikiwa na kuleteta matoke finyu."
Dhumuni la mkutano huo, ilikuwa ni kuzungumzia hali halisi ya maswala ya kinyukli yanavyoendeshwa nchini Iran, lakini hakuna ufumbuzi uliofikiwa.
Picha hapo juu anaonekana Saeed Jalili mkuu wa maswala ya kinyuklia wa Iran, akitoka katika ukumbi wa mkutano, mara baada ya kumaliza mazungumzo.

1 comment:

chib said...

Mwanzilishi wa mtandao wa wikiLeaks, sasa wameamua kumtia kitanzi cha ubakaji!!