Tuesday, December 28, 2010

Laurent Gbagbo akutana na viongozi wa ECOWAS.

Laurent Gbagbo akutana na viongozi wa ECOWAS.

Abidjan, Ivory Coast- 28/12/2010. Marais watatu wa jumuia ya kiuchumi ya nchi za Afrika ya Magharibi wamekutana na rais wa Ivoty Coast ili kujadili hali ya kisiasa nchini humo na kumtaka aachie madaraka. Marais hao ni Boni Yayi wa Benin, Ernest Bai wa Sierra Leone, na Pedro Pires wa Kape Verde walikutana na rais wa sasa Laurant Gbagbo kuzungumzia hali halisi ya myumbo wa kisiasa uliopo katika nchi hiyo. Marais hao kabla ya kuonana na Gbagbo, waliongea na Alassane Ouattara ambaye jumuia ya kimataifa inamtambua kama ndiye mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika hivi karibuni. Hata hivyo hakuna habari zilizo tolewa kwa undani ili kwa pamoja walisema mkutano ulikuwa wa mafanikio. Picha hapo juu wanaonekana marais wa Laurent Gbagbo kushoto, Ernest Bai Koroma wa Sierra Leone na Boni Yayi wa Benin wakiongea na waandishi wahabari mara baada ya kukutana kwao.
Urussi yazitaka nchi nyingine kuangalia mambo yao.
Moscow, Urussi - 28/12/2010. Serikali ya Urussi imezitaka serikali za nchi nyingine kutoingilia mambo yake na nchi hizo zitizame maswala ya nchi zao.
Uamuzi wa serikali ya Urussi kutoa tamko hilo umekuja mara baada ya baadhi ya nchi zikiongozwa na Amerika kulaumu kitendo cha mahakama nchini Urussi kumkuta na hatia Mikhail Khodorkovsky kwa kosa la kutumia mali na pesa za nchi kinyume cha sheria .
Waziri wa mambo ya nje wa Amerika Hillary Clinton, alisema " kitendo cha kuhukumiwa kwa Mikhail kinaleta mashaka kutokana na jinsi kesi hiyo ilivyo endesshwa."
Picha hapo juu anaonekana Mikhail Khodorkovsky akisikiliza hukumu ilipo kuwa inatolewa mbele yake.

No comments: