Monday, April 11, 2011

Jeshi la Alassane Ouattara la mkamata Laurent Gbagbo.

Jeshi la Alassane Ouattara la mkamata Laurent Gbagbo. Abidjan, Ivory Coast -11/04/2011.Jeshi la upinzani linalo ongozwa na Alassane Ouattara, kwa kushirikiana na jeshi la Ufaransa limefanikiwa kumkamata aliyekuwa rais wa Ivory Coast baada ya kuvamia makazi yake.

Rais huyo wa Ivory Coast Laurent Gbagbo,alikamatwa baada ya mashambulizi kati ja jeshi lake na jeshi la Ouattara kwa msaada wa Ufaransa na vifaru huku helkopta zikisaidia kuhakisha ya kuwa Gbagbo na jeshi lake hawawezi kuendeleza mashambulizi.
Msemaji wa Alassane Ouattara, Affaoussy Bamba alisema, " Laurent Gbagbo amekamatwa na sasa yupo mokononi mwa jeshi letu.
Hata hivyo , msemaji wa Laurent GbagboToussaint Alain , alisema jeshi la Ufaransa limemkamata Gbagbo baada ya kuvamia makazi yake.
Kufuatia madai hayo, waziri wa ulinzi wa Ufaransa alikanusha madai hayo na kusema ,"Gbagbo alikamatwa na jeshi la Alassane Ouattara."
Kukamatwa huko kwa Laurent Gbagbo, kumekuja baada ya rais huyo kudai yakuwa yeye ndiye mshindi wa matokeo ya uchaguzi, na huku mpinzani wake Alassane Ouattara akidai yeye pia ameshinda uchaguzi na umoja wa mataifa kuunga mkono.
Kundi la upinzani la kataa mpango wa kuleta amani nchini Libya.
Benghazi, Libya - 11/04/2011. Kundi la upinzani linalopigana na serikali ya Libya limepinga mpango uliopitishwa na umoja wa Africa ili kusimamisha mapigano.
Msemaji wa kundo hilo lili na makao yake makuu Benghazi, Mustafa Jabiri alisema " hatuwezi kushirikiana na uongozi wa Muammar Gaddafi, na lazima uachie madaraka yeye na familia zao, na tutakufa nao au tuchukue ushindi kwa mtutu wa bunduki."
Uamuzi wa kundi hilo kukataa mpango wa umoja wa Africa ili kuleta amani kati ya serikali ya Libya na wapinzani wake ulikuja baada ya viongozi wa jumuia hiyo chini ya rais wa Afrika ya Kusini Jacob Zuma kukutana na Muammar Gaddafi ili kujadili mpango wa kuleta amani.

No comments: