Monday, April 23, 2012

Nchi za jumuiya ya Ulaya zaondoa vikwazo kwa Myanmar.

Korea ya Kaskazini yaitaadhalisha Korea ya Kusini.


Pyongyang, Korea ya Kaskazini - 23/04/2012. Serikali ya Kora ya Kaskazini imetishia ya kuwa inauwezo wa kuisambaza serikali ya Korea ya Kusini kwa muda wa dakika nne.
Habari kutoka serikali ya Pyongyang zilisema kupitia luninga ya taifa " tunauwezo wa kuizamabaza Korea ya Kusini kwa madakika ikiwa majaribio ya mashambulizi yatafanywa katika maeneo ya nchi yetu."
Hali ya mvutanao wa kimalumbano kati ya Korea ya Kaskazini na Kusini zimetokea baada ya Korea ya Kaskazini kutofanikwa kurusha chombo cha kisayansi angani ambacho ilitarajia kukitumia kwa njia ya mawasiliano..


Nchi za jumuiya ya Ulaya zaondoa vikwazo kwa Myanmar.


Brussels, Ubeligiji - 23/04/2012.  Jumuia ya nchi za Ulaya EU zimekubaliana kwa pamoja kuitolea vikwazo nchi ya Myanmar ambavyo vilikuwa vimewekwa kwa muda mrefu.
Uamuzi huo wa nchi za jumuia ya Ulaya EU umekuja baada ya mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizo walipo kutana Luxembourg.
Habari kutoka katika mkutano huo zinasema " hali inaanza kuwa ya kuridhisha nchi Myanmar, kwani wameonesha ngazi moja ya mageuzi ya kisiasa na kuna matumaini ya kuwa serikali iliyopo itaendelea kuleta magauzi bora."
Hata hivyo siyo vikwazo vyote vilivyo ondolewa, "bali vikwazo vya kuiuzia siraha Myanmar bado vitasimama palepale" ziliongezea habari kutoka mkutano huo.
Kutangazwa kwa kuondolewa vikwazo hivyo kwa nchi ya Myanmar kumekuja baada ya waziri mkuu wa Uingereza David Cameron kufanya ziara ya kiserikali nchi humo hivi karibuni, na kuweza kufanya mazungumzo na kiongozi wa upinzani Aung  Suu Kyi, ambaye alikuwa chini ya kifungo cha nyumbani kwa miaka miaka mingi.

Misri yasimamisha kuiuzia Izrael gasi.


Kairo, Misri - 23/04/2012. Shirika linalo sambaza na mushughulikia masi nchini Misri limetangaza kusimamisha uuzaji wa gasi nchi Izrael kuanzai sasa.
Mohamed Shoeb ambaye ni msemaji wa kampuni ya usambazaji gasi nchini Misri - Egypt Natural Gas Company alisema " tumeamua kusimamisha uuzaji wa gasi nchini Izrael na uamuzi huo ni wa kibiashara na wala si wakisiasa."
Waziri wa fedha wa Izrael Yuval Steinitz alisema " uamuzi wa Misri kusimamisha uuzaji wa gasi ni wa kuangaliwa kwa makini kisiasa na kiuchumi.
"Hii ni hatari kwani kunakiuka mkataba wa amani na utulivu iliyopo kati ya Izreal na Misri na uamuzi huo siyo mzuri na haufai."
Swala la uuzaji wa gasi kati ya Misri na Izrael uliingia dosari mara baada ya kuangushwa serikali ya rais Husni Mubaraka, ambapo serikali yake ilikuwa na mawasiliano mazuri na serikali ya Izreal tangu achukue madaraka ya urais 1981.


Rais wa Sudan adai ni mtutu wa bunduki ni lugha itakayo tumika  kuanzi sasa.


Khartoum, Sudan - 23/04/2012. Rais wa Sudan amekataa kuwepo na usuruhishi na majadiliano ya kuleta amani kati ya serikali yake na serikali ya Sudani ya Kusini.
Rais Omar al Bashir alisema "hatuwezi kujadiliana na kusuruhishana na serikali ya Sudani ya Kusini, kwan awaelewi kitu, ila msemo wa mtutu bunduki ndiyo lugha wanayo elewa.
"Na mazungumzo yetu kwano ni mtutu uliyo jaa sisasi."
Shirika la habari la serikali ya Sudan limesema jeshi la serikali limefanikiwa kuwaua wanajeshi 1,200 wa jeshi la Sudan ya Kusini wakati wamapambano yaliyo tokea hivi karibuni.
Mzozo kati ya Serikali ya Sudani ya Kusini na Sudani  ulianza hivi karibuni kutokana na tatizo la mpaka kati ya nchi hizo mbili ambapo inasemekana kuna utajiri wa mafuta.

No comments: