Sunday, April 8, 2012

Joyce Banda aapishwa kuwa rais wa Malawi.

Mamia waudhuria misa ya Pasaka Vatican City.

Vatican City, Vatican - 08/04/2012. Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani ameongoza misa ya sikukuu ya Pasaka na kwa kuomba amani na utulivu kutawa nyoyo za binadamu.
Papa Benedikt XVI akiongoza misa alisema" tukiwa tunasherekea kufufuka kwa Yesu Kristu aliyeshinda mauti, tunaomba ufufuo wake ulete amani  kwenye maeneo yote duniani yanayo kabaliwa na vita na ukame.
Kuanzia nchi za Mashariki ya Kati, Syria, Izrael Palestina Irak na kwa wale wote walio kumbwa na matatizo ya vurugu katika bara la Afrika."
Papa Benedikt pia aliwatakiwa waumini wote duniani Pasaka njema yenye furaha na amani.
Siku ya leo Wakristu duniani kote wansherekea siku ambayo Yesu Kristu alifufuka baada ya kuhukumiwa na Pilato na baadaye kutundikwa msalabani ili maandiko yatimie.

Joyce Banda aapishwa kuwa rais wa Malawi.
Lilongwe, Malawi - 08/04/2012. Makamu wa rais wa Malawi ameapishwa kuwa rais wa nchi hiyo kufuatia kifo cha rais Bingu wa Mutharika  kilichotokea siku ya 05/04/2012.
Joyce Banda 61, atakuwa rais wa kwanza mwanamke kuchukua madaraka hayo ya juu ya kuongoza nchi  Malawi na katika ukanda wa Kusini na Mashariki ya Afriaka.
Rais Joyce Banda alisema haya baada ya kuapishwa "nitafanya kazi yangu kama inavyo sema katiba ya nchi na kuitumikia Malawi kwa moyo wangu wote, na napenda tuwe na matumaini mema na umoja, kwa imani naamini hakutakuwa na mwanya wa kulipizana visasi, na kwakuwa sisi ni taifa linalo muamini Mungu basi hatutashindwa kutimiza aliyo agiza."
Rais Banda alisisitiza utulivu hasa katika kipindi hiki cha malombelezi ya kuondokewa na aliye kuwa rais wa Malawi Bingu wa Mutharika.

Uingereza yapiga marufuku kuweka wazi sigara madukani.

London, Uingereza - 08/04/2012. Serikali ya Uingereza imepiga marufuku na kuagiza maduka yote nchini humo kuziba na kufunika sigara zilizopo madukani.
Kwa mujibu wa habari kutoka serikalini zinasema "kwa kuziba na kufunika sigara zilizopo madukani kutasaidia kupunguza kishawishi cha kuvuta sigara na vilevile huenda tabia ya kuona sigara na kutaka kuvuta ikapungua."
hata hivyo baadi ya wafanyabiashara na raia wamesema "kitendo hicho hakita saidia kwani kila mvuta sigara anajua nini sigara gani anavuta."
Uamuzi huo wa serikali ya Uingereza kupiga marufuku kuweka sigara wazi madukani umekuja baada ya kampeni kubwa ya kupambana na magonjwa yanayo husiana na uvutaji wa sigara kuongezeka.

No comments: