Friday, June 22, 2012

China na Brazil kubadilishana pesa kibiashara.

Rais wa Afghanistan ashutumiwa kwa undugu.

Kabul, Afghanistan - 22/06/2012. Rais wa Afghanistan amekubwa na wakati mgumu, baada ya kujulikana  ya kuwa binamu yake amepewa tenda ya kuchimba mafuta yaliyopo nchini humo.
Rais Hamid Karzai amekumbwa na shutuma hizo, baada ya  ya binamu yake ambaye anaye miliki kampuni ya Rashi na Reteb Popal kupewa tenda ya kuchimba mafuta pamoja na kampuni moja toka Uchina.
Binamu huyo wa rais Karzai, ambaye alishawahi kufungwa nchini Marekani kwa makosa ya kusafirisha na kuuza madawa ya kulevya  miaka ya 1990s, amepatiwa mkataba kuchimba mafuta yaliyopo katika bonde la Amu Darya kwa miaka 25.
Nchi ya Afghanistan inaaminiwa kuwa na madini tofuti yenya thamani, mafuta na gasi yenye kufikia kiasi cha paund za Uingereza  £2trillion.
China na Brazil kubadilishana pesa kibiashara.
Rio de Janeiro, Brazil - 22/06/2012. Serikali za China na Brazil zimekubalia kubadilishana pesa za kupitia banki kuu za nchi hizo.
Uamuzi huo umekuja baada ya viongozi wa nchi hizo hao kukaa na kujadili ni mbinu gani zifanyike ili kudhibiti myumbo wa kifedha kati ya nchi hizo mbili.
Mabadilishano hayo ya fedha ambayo yata ziruhusu nchi hizo mbili kubadilishana kiasi cha 60billion Brazilian reais na 190 China yuan sawasawa na paundi za Uingereza 31billion, jambo ambalo litafanya nchi hizo kuweza kufanya biashara bila vikwazo kati ya nchi hizo.
Wabunge nchi Zimbabwe wakubali kutailiwa. 
Harare, Zimbabwe -22.06/2012. Baadhi ya wabunge nchini Zimbabwe wamekubali kutailiwa ili kuwa mfano mzuri kwa wananchi ikiwa katika harakati za kupambana  ugonjwa wa ukimwi.
 Blessing Chebundo  ambaye ni Mwenyekiti wa bunge la Zimbabwe alisema " nivizuri kwa wabunge kuonyesha mfano, kwani sisi sote tupo katika harakati ya kupambana na ugonjwa wa ukimwi na kama viongozi ni muhimu kuonye mfano bora kwa wananchi."
Kampeni ya kuwataka viongozi wawe mfano bora wa kupambana na ukimwi ilianzishwa na makamu wa waziri mkuu Bi Thokozani Khupe mwaka 2011.
Uamuzi wa wabunge hao kuamua kutailiwa kumekuja baada ya wachunguzi wa maswala ya kiafya kutoa ripoti ya kuwa mtu aliye tailiwa hana hatari ya kuambukiza ugonjwa wa ukimwi kiurahisi.

Uingereza yamnyima viza mkuu wa Olyimpik wa Syria.
Islamabad, Pakinstan - 22/06/2012. Serikali ya Uingereza imekataa kumpa viza mkuu wa  michezo ya Olyimpik wa Syria.
Mowaffak Joumaa ambaye pia ni mkuu wa jeshi, amekataliwa viza ya kuingia nchini Uingereza kwenye michezo ya kimataifa ya Olyimpik itakayo fanyika hivi karibuni.
Habari zilizo patikana zinasema "uamuzi huo ulichukuliwa katika kikao kilicho fanyika kati ya wakuu wa ofisi ya mambo ya nje ya nchi na wizara ya michezo na utamaduni."
Uamuzi huo wa serikali ya Uingereza kumyima viza mkuu huyo wa maswla ya Olyimpik wa  wa Syria utakabidhishwa kwa viongozi wanaosimamia michezo ya Olyimpik siku chache kuanzia sasa.
Swala la Serikali ya Uingereza kumkatalia viza ya kuingia mkuu huyo wa Syria, umekuja kutoka na mvutano wa kidiplomasia uliyopo kati ya nchi hizi mbili.

No comments: