Saturday, June 2, 2012

Hosni Mubaraka ahukumiwa kukaa jela maisha.

Hosni Mubaraka ahukumiwa kukaa jela maisha.

Kairo, Misri - 02/06/2012. Aliyekuwa rais wa Misri amehukumiwa kukaa jela maisha, baada ya kukutwa na hatia ya kushindwa kusimamisha vurugu zilizo pelekea mauaji ya raia.
Hosni Mubaraka 84 alihukumiwa adhabu hiyo, yeye pamoja na aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani Habib al Adli.
Hosni Mubaraka ambaye alitolewa madarakani baada ya mapinduzi ya maandamano yaliyo fanyika Februari  2011 kufuatia mlolongo wa mapinduzi ya kisiasa yaliyoko katika maeneoa ya nchi za Kiarabu.

Putin akanusha ya kuwa Urusi yaisaidia serikali ya Syria.

Berlin, Ujerumani - 02/06/2012. Rais wa Urusi amekanusha  ya kuwa Urusi inaiunga mkono serikali ya Syria.
Rais Vladmir Putin ambaye  amefanya zaiara  nchini Ujerumani na ya nje ya nchi kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kuwa rais wa nchi hiyo.
Akiwa ziarani nchi Ujerumani Putini alisema " Urusi haiungi mkono upande wowote wa matatizo ya Syria, ila tunachounga mkono ni mpango wa Kofi Annan."
Rais Putin aliyasema hayo baada ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton kudai ya kuwa Urusi inaisadia serikali ya Syria na ndomaana hali inazidi kuwa mbaya nchi humo. 
Putin alikutana na Kansera wa Ujerumani Angela Markel  na kukubaliana kwa pamoja ya kuwa ya kuwa swala la Syria lazima lisuruhishwe kwa kupita mazungumzo na siyo vita..

Ban Ki-moon aagiza Somalia kupatiwa msaada zaidi wa kiusalama.

Instambul, Uturuki - 02/06/2012. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ameagiza jumuiya ya kimataifa kuisaidia serikali ya  mpito ya Somalia katika kujenga nchi japo inakabiliwa na wakati mgumu.
Ban Ki-moon alisema "swala la usalama wa Wasomalia lazima lizidishwe nguvu kutoka pande zote za jumuiya ya kimataifa ili Somalia irudi iweze kurudi kuwa nchi ya maendeleo ya mazuri."
Mkutano huo, ambao uliitishwa ili kuangalia ni kwa kiasi gani jumuiya ya kimataifa inaweza kuisaidia Somalia, na hasa katika swala la kuleta amani nchini humo.
Serikali ya mpito ya Somalia imekuwa ikipambana na kundi la Al Shabab, ambalo linapingana naserikali hiyo ya mpito na kusababisha hali ya usalama kuwa tete na wanachi kushindwa kuijenga nchi.

No comments: