Thursday, June 28, 2012

Watu 40 wapoteza maisha katika lori baada ya kukusa hewa.

Ururiki yapeleka majeshi yake kwenye mpaka na Syria.


Ankara, Uturuki - 28/06/2012. Serikali ya Uturuki imeamua kuimarisha ulinzi katika mipaka yake na Syria kwa kuamua  kupeleka siraha  na wanajeshi mpakani na nchi hiyo kufuatia kuangushwa kwa ndege yake ya kivita  hivi karibuni na Syria.
Siraha hizo ambazo ni  za kutungulia ndege na za kuzuia mabomu zimlipelekwa kwenye mpaka na Syria baada la  tamko la serikali ya kuwa hawataruhusu tena kitendo hicho kutokea.
Kutokuelewana kati ya Syria na Uturuki kumekuja baada ya serikali ya Uturuki kuwaunga mkono na kuwahifadhi wapinzani waserikali ya Syria ambao kwa sasa wanapambana kivita na serikali ya Syria.

Benki maharufu duniani yapigwa faini.

London, Uingereza - 28/06/2012. Benki ya Barclays nchini Uingereza imepigwa faini kwa makosa ya kukiuka misingi ya mikopo na kupandisha riba.
Benki ya Barclays ilipigwa faini kiasi cha $453millioni dola za Kimarekani  baada ya wachunguzi wa maswala ya masoko fedha na mikopo kugundua ya kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa masharti na maadili ya kibenki.
Hali hii ya  benki ya Barclays kupigwa faini imezidi kuleta msuguano mkubwa nchini Uingereza, kufuatia uamuzi wa serikali uliyo ufanya hapo wali kwa kuzisaidia benki kifedha baada ya benki hizo kuyumba kibiashara. 

China yakamulisha harakati za kianga kwa njia ya kawaida.

Beijing, China - 29/07/2012. Wanaanga watatu wa wa Kichina wamerudi duniani baada ya kumaliza  harakati zao za kisayansi katika anga (orbit)
Wanasayansi hao watatu ambao kati yao alikuwa mwanamke na  walitumia vyombo ambavyo vilikuwa vinaongozwa kwa njia ya kawaida (manual),  walitua duniani bila matatatizo yoyote kwa mujibu wa habari kutoka serikali ya Uchina.
China imewarusha wanaanga hao kufuatia kitendo kama hicho kilicho fanywa na Marekani na Urusi miaka ya sitini.

Watu 40 wapoteza maisha katika lori baada ya kukusa hewa.

Dodoma, Tanzania - 28/06/2012. Polisi nchini Tanzania wamewakuta watu wapatao 40 wamekufaa ndani ya lori lililo kuwa limewabeba.
Watu hao 40 ambao walikuwa raia wa Somalia na Ethiopia walikufa kutokanaa na kukosa hewa ndani ya lori hilo ambalo walikuwa wanasafiria na  halikujulikana lilikuwaa limetokea sehemu gani na watu hawa.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa  Tanzania Isaac Nantanga alisema " kumekuwa na ongezeko la watu kutoka Somalia na Ethiopia ambao wamekuwa wakielekea nchini Afrika ya Kusini kutokana hali zilizopo katika nchi hizo."
Usafirishwaji wa watu katika  malori umekuwa ukitumika sana katika baadhi yaa nchi za Afrika jambo ambalo limekuwa likihatarisha maisha ya watu wanao tumia maroli hayo.

No comments: