Monday, June 4, 2012

Wananchi wa Uingereza washerekea pamoja na Malkia kwa kutimiza miaka 60 ya Umalkia.



London, Uingereza - 04/06/2012. Wananchi wa Uingereza wapo wanamesherekea sikuku ya kutimiza miaka 60 ya  utawala wa Malkia Elizabeth tangu atawazwe kuwa Malkia wa Uingereza.
Sikuku hiyo iliyopewa jina Diamond Jubiles, ambayo itachukuwa siku mbili kwa kuanza tarehe 03/06/2012 na kuishia 04/06/2012, ilishangiliwa kwa pamoja na Malkia Elizabeth huku akiwa ndani ya boti iliyokuwa ikipita katika mto mkubwa unao julikana kwa jina la Thames uliyopo jijini London ikiwa ni moja ya njia ya kuadhimisha sherehe ya miaka 60.
Malkia Elizabeth amekuwa mmoja ya  Malkia walio kaa katika kiti cha Umalkia kwa muda mrefu kulinganishana na viongozi wengine wa Kifalme waliopo duniani. 

Kiongozi wa Iran adai Iran inanguvu zaidi kuliko miaka ya nyuma.

 Tehran, Iran - 04/06/2012. Kiongozi mkuu wa Iran ametangaza ya kuwa Iran ina nguvu za kutosha kulinganisha na miaka ya nyuma.
Ayatollah Sayyed Ali Khamenei akiongea katika siku ya kumkumbuka ya kutimiza miaka 23 ya  kiongozi aliye ongoza mapinduzi Ayatollah Sayyed Rouhallah Khomeini kwa kusema " leo Iran inanguvu kulinganisha na miaka ya nyuma iliyopita baada ya mapinduzi na maadui wanaiogopa Iran siyo kwa nguvu za kinyuklia bali kama Iran nchi ya Kiislaam.
"Nguvu ilizo nazo irani ni za kisiasa na ushawishi mkubwa katika kuhamasisha nchi za jumuiya ya kimataifa ili kujijenga zenyewe na Iran haita tengeneza bomu la nyuklia kamwe."
Mazungumzo hayo ya kiongozi huyo mkuu wa Iran yamekuja huku mazungumzo ya kuhusu Iran na mradi wa kinyuklia kuisha hivi karibuni nchini Irak bila kufukia maaafikiano.


Ajali ya ndege yaua watu 153 nchini Nigeria.

Lagos, Nigeria - 04/06/2012. Watu wapatao 153 wamepoteza maisha baada ya ndege iliyo kuwa imewabeba kugonga maghorofa yanayokaliwa na raia katika jiji la Lagos.
Horald Denuren ambaye ni msemaji wa maswala ya anga alisema " ndege ambayo ilikuwa ikitokea Abuja kuja Lagos imeaanguka na kupoteza maisha ya watu  na pia kusababisha uharibifu mkubwa katika eneo iliyo anguka ndege hiyo."
Kufuatia ajali hiyo, rais wa Nigeria ametangaza siku tatu za maombelezi kutoka na vifo vya vilivyo sababishwa  na ajali hiyo ya ndege.
Ajali hiyo ya ndege nchini Nigeria inafuatia ajali ya ndege iliyotokea nchi ya jirani ya Ghana na kuuwa watu kumi baada ya ndege hiyo kutua kwenye kituo cha mabasi kilichopo karibu na uwanja wa ndege.

Rais Bashar al Assada adai nguvu za kutoka nje zinavuruga amani.

Damascus, Syria - 04/06/2012.  Rais wa Syria amehutubia  baraza la bunge jipya wakati hali ya kiusalama inazidi kuzorota  nchi Syria na kuashiria hali ya kuzuka vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Rais Bashar al Assad akihutubia bunge alisema " Syria ipo katika vita vinavyo sababishwa kwa nguvu kutoka nje ya nchi na mauaji yaliyo tokea hivi karibubi huko Haula yamefanywa na watu wenye roho za kinyama na wasio na utu.
"Tunapigana na ugaidi lakini vita vyote vinapangwa na kupiganwa nchi mwetu na damu za Wasyiria kumwagika hata hivyo tutashinda vita zidi ya ugaidi huo."Bashar al Assad aliyasema hayo wakati alipo kuwa akongea na  wabunge waliochaguliwa hivi karibuni.

No comments: