Saturday, June 23, 2012

Marekani yatoa onyo la mashambulizi katika mji wa Mombasa.

Serikali ya Uganda kupiga marufuku wapenzi wa jinsia moja.

Kampala, Uganda - 23/06/2012. Serikali ya Uganda imezifuta ofisi na mashirika yasiyo yanayo husika katika kuunga mkono ushoga na watu wanao pendana kwa jinsia moja.
Waziri Simon Lokodo ambaye ni waziri wa maadili ya jamii alisema "  pendekezo la kuzisimamisha na kuzifuta ofisi hizo  zimekuja baada ya mimi  kuangalia kiundani na bila kuwa na shaka ya kiubinadamu yakuwa  mashirika  haya 38 yanahusika katika kampeni ya kukuza ushoga, jambo ambalo ni kinyume na maadili yetu na kiimani.
Kampeni hya kuponga ushoga nchini Uganda, imekuwa ikikua siku hadi siku, na kuungwa mkono na wakuu wa dini nchini humo.


Marekani yatoa onyo la mashambulizi katika mji wa Mombasa.


Mombasa, Kenya - 23/06/2012. Mji wa Mombasa umeongezewa ulinzi baada ya ofisi za ubalozi wa Marekani kuaagiza  raia wake waliopo katika mji huo kuondoka.
Uamuzi wa Marekani kuaagiza raia wake kuondoka katika mji wa Mombasa, umekuja baada ya kupata habari ya kuwa "bandari iliyopo katika mji huo, inaweza shambuliwa muda wowote."
Nayo serikali ya Ufaransa imewataka wananchi wake kuwa waangalifu kwa kipindi chote watakapo kuwa katika mji huo wa Mombasa.
Hata hivyo maafisa usalama wa Kenya kwa kushirikiana na polisi, wameeomba "kuwepo na utulivu kwani wanafuatilia habari hizo."
Kenya imekuwa ikikimbwa na mashambulizi ya mabomu kwa muda zaidi ya mwaka mmoja, tangu serikali hiyo ilipo amua kupambana na kundi la Al Shabab nchini Somalia, na kundi la Al Shabab kuhaidi kufanya mashambulizi nchi Kenya ikiwa ni njia ya kulipiza kisasi.


Syria yaangusha ndege ya kijeshi ya Uturuki.


Ankara, Uturuki - 23/06/2012. Serikali ya Uturuki imedandege  iliyoangushwa  na jeshi la Syria ni ndege yake ya  kivita.
Kwa mujibu wa habari kutoka jeshi la Syria, zinasema " ndege hiyo ilivuka mpaka na kuingia ndani ya  anga za Syria na jambo ambalo ililazimisha jeshi hilo kuiangusha ndege hiyo."
Nayo serikali ya Uturuki imedai ya kuwa kitendo cha kuingusha ndege yake, sikitendo cha kuchukuliwa juju juju, na bado inafanya uchunguzi ili kujua ukweli kamili, na itafanya uamuzi baada ya uchunguzi kuisha. 

1 comment:

Anonymous said...

OUT OF TOPIC
ZAMARADI nimetazama kipindi chako jana siju nicoment wap ktk bongo movie, ila yule binti hukupaswa kumuanika hadharani vile maisha yake yatakuaje? je ingekua wewe ungefurah ?ukiwa kama dada kuna vtu ungepaswa umuulize kwanza maana bado mdogo na haelewi chochote kuhusu utandawaz kashachanganyikiwa na maisha.ungemficha sura naelewa unataka msaidia laikn unapaswa fikiria sana kabla hujarusha kpndi chako.jamii itampokeaje na watu hua wana mawazo tofauti ile itakua ni kashfa ktk maisha yake yote. kulala na wanaume 30 naamin itamgarim na atajuta kijitangaza