Wednesday, June 20, 2012

Viongozi wa Somalia kufanya mkuutano wa kuungana.

Viongozi wa Somalia kufanya mkuutano wa kuungana.


London, Uingereza - 20/06/2012. Wakuu wa Somaliland na Somalia wanatarajiwa kufanya mazungumzo nchini Uingereza ili kuweza kuzungumzia jinsi ya kuunganisha nchi hizo.
Mazungumzo hao ambayo wanatarajiwa kufanyaka nchini Uingereza London katika sehemu ambayo haijatajwa yanania ya kuiwezesha Somalia na Somaliland kuwa  Jamuhuri au kuwa nchi moja.
Somalialanda imekuwa na amani tangu kuanguka kwa serikali ya rais Muahmad Siad Barre 1991, huku upande wa Somalia ya Kusini Mogadishu umekumbwa na machafuko ya kutokuwa na amani na vita ambavyo vimeleta  athari kubwa kwa watu na mazingira.

Mkutano wa G20 nchini Mexico wamalizika.

Los Cobos, Mexico - 20/06/2012. Wakuu wa nchi zilizo tajiri na zile  zinazo kua  kiuchumi wamemaliza kikao na kuagiza kukuza uchumi na kuongeza ajira.
Wakuu hao ambao wa mekubaliana kwa pamoja ya kuwa uchumi wa dunia umepata changamoto katika kila nyaja na ipo haja ya kutumia kila mbinu ili kuimalisha hali ya uchumi wa dunia na kuinua maisha ya raia wa kila nchi.
Mkutano huu umekuja wakati myumbo wa uchumi duniani umekuwa ikiwapa vichwa kuuma wakuuwa nchi kila wanapo kutana tangu mwaka 2008 na hadi sasa bado wanajaribu kutafutia jibu sahihi, 
Julian Assange achukua ukimbizi ubalozi wa Ekuado.

London, Uingereza - 20/06/2012. Mwanzilishi wa mtandao wa Wikileaks amekimbilia ubalozi wa Ekuado uliyopo Uingereza na kuomba ukimbizi.
Julian Assange aliomba ukimbizi kweye ubalozi wa Ekuado jana, baada ya rufaa yake ya kutaka kesi inayo mkabili ya ubakaji isikilizwe upya kukataliwa na mahakama  nchini Uingereza.
Vaunghan Smith ambaye ni rafiki wa Julian Assange alisema " Assange anaogopo kwani akirudishwa Sweden kunauwezekano mkubwa akapelekwa Marekani, kwani anatakiwa na nchi hiyo kwa kutoa siri za nchi hiyo."
Julian Assange anakabiliwa na kesi ya ubakaji nchini Sweden, jambo ambalo amekanusha na alikuwa amewekewa dhamana na watu wake wakaribu ambao hata wao wanadai kushutushwa na kitendo hicho cha kuchukua ukimbi katika balozi za Equado zilizopo London  nchi Uingereza.

Hatimaye Ugiriki yapata serikali.

Athens, Ugiriki -20/06/2012. Wananchi wa Ugiriki wapeta serikali baada ya uchaguzi ambao ulitoa mgwanyo wa matokeo ambao ulifanya serikali ya shirikisho kuundwa.
Antonis Samaras 16 aliyekuwa mshidi kupitia chama cha New Democras Part ameapishwa kuwa waziri mkuu wa Ugiriki baada ya kukubaliana kuunga serikali na chama cha Greece's socialist PASOK.
 Waziri Mkuu Antonis Samaras anakabiliwa na kazi ngumu ya kuhakikisha uchumi wa Ugiriki unarudi katika hali ya kawaida na huku kukubali matwakwa  yaliyoamliwa na nchi za muungano wa Ulaya ya kuwa ili Ugiriki ipatiwe pesa za kuinua uchumi, ni lazima ifanye mabadiliko ya miundo uchumi kwa kubana matumizi katika sekta tofauti jambo ambalo baadhi ya wanchi wa Ugiriki wanalipinga.

No comments: