Wednesday, June 6, 2012

Marekani kutafuta mshiriki mpya kiulizi.

Viongozi wa nchi za Pasifiki na Asia ya kati wakutana nchini China.

Shanghai, China - 06/06/2012.  Viongozi wa nchi za Pasifiki na Asia ya Kati wamekutana nchini China ili kuzungumzia maswala ya  ulinzi , usalama na kukuza ushirikiano wa kiuchumi.
Mkutano huo ambao watakuwepo viongozi na  marais wa Urusi, Iran na wengine ulisimamiwa na rais wa China  Hu Jintao ambaye ni rais mwenyeji.
Rais wa China Hu Jintao alisema " tutaendelea kujenga na kulinda eneo letu, japo kutakuwa na nguvu kutoka nje ya maeneo ya yetu,  na tutashinda.
Na tutafanya kila njia amani inapatikana nchi Afghanistan." Aliongezea rais Hu Jintao.
Mkutano huo unao julikana kama Shanghai Cooparation Organization umetimiza miaka 12 tangu kuanziashwa kwa madhumuni ya kuimairisha uhusiano wa karibu wa nchi zilizopo  katika maeneo ya Pasifiki na Asia ya Kati.

Marekani kutafuta mshiriki mpya kiulizi.

New Dheli, India - 06/06/2012. Waziri wa Ulinzi wa Marekani amefanya ziara ya kiserikali nchini India na kuzungumza na viongozi wa India kuhusu maswala ya kiulinzi na usalama kati ya nchi hizo mbili.
Ziara ya Waziri Leon Panetta inachukuliwa " ikiwa ni moja ya sera za kiulinzi za  Marekani ili kupata mshiriki mpya katika eneo la India na Pasifiki, baada ya uhusiano wa Marekani na Pakistani kuonekana kuyumba." alisema George Little ambaye ni mmoja  wa msemaji  wa Pentagon.
India imekuwa nchi ambayo inakuwa kiuchumi na kiulinzi na kuvutia mahusiano na nchi zenye nguvu kijeshi kama Urusi na China  hivi karibuni. 

Al Qaeda yapata pigo.

Washington, Marekani - 06/06/2012. Serikali ya Marekani imethibitisha ya kuwa mmjo wa viongozi wakuu wa kundi la Alqaeda ameuwawa.
Habari zilisema "Abu Yahya al Libi aliuwawa na baada ya ndege ya aina ya drone kushambulia eneo alilo kuwa amejificha.
Kifo cha Libi ni pigo kubwa kwa kundi hilo la Al Qaeda, kwani alikuwa ni mtu anaye panga mipingo ya kundi hilo." Ikulu ya Marekani ilisema."
Kuu wawa kwa viongozi wa kundi la Al Qaeda kumekuwa kukiendelea na kundi hili ndilo linalo husika katika ugaidi.

Malkia Elizabeth atoa shukurani kwa watu wote. 

London, Uingereza - 06/06/2012. Malkia Elizabeth wa Uingereza  ameanda chakula cha mchana na viongozi wa nchi Commowealth ikiwa ni moja ya katika sherehe za kuadhimisha miaka 60 tangu atawazwe kuwa Malikia.
Malkia Elizabeth aliwashukuru watu wote walio kuwa pamoja naye kisala na furaha katika uongozi wake na siku hii ambayo amefikisha miaka 60 ya Umalkia.
Sherehe hiyo ya pamoja kati ya Malkia Elizabeth na viongozi wa Commonwealth itafanyika katika ukumbi wa Marlborough Pall Hall uliyopo katika ya jiji la London ikiwa ni moja ya ishara ya kuwashukuru viongozi hao wa nchi ambazo zilitawaliwa na Mwingereza.
Malkia  Elizabeth wa Uingereza ni kiongozi wa kwanza katika karne ya hii kukaa katika madaraka kwa muda wa miaka 60, na sherehe hizo zilimalizika 05/06/2012, ambapo mamilioni ya Waingereza waliungana na Malkia kusherekea sikuku hiyo.

1 comment:

Anonymous said...

buy valium average street price valium - buy roche valium online