Sunday, June 17, 2012

Mahakama ya Kimataifa yapata mwanasheria mkuu Mwafrika.

Kamati ya kusimamia usalama na amani nchini Syria yasimamisha kaza zake.


Damascus, Syria - 17/06/2012. Mkuu wa wa kamati iliyo teuliwa na umoja wa mataifa ya kusimamia hali ya kuwepo kwa usalama na kurudisha amani ametangaza kusimamisha huduma zote za kamati hiyo nchini Syria.
Meja Generali Robert Mood akiongea na waandishi wa habari alisema "kamati ya umoja wa mataifa inayosimamia kuletwa kwa usalama nchini Syria imesimamisha kazi zake kufuatia hali ya usalama kwa wafanyakazi wake kuwa katika hali ya hatari."
Wasimamizi wapatao 300 ambao walikuwa na kazi ya kuhakikisha hali ya usalama nchini Syria wamekuwa na wakati mgumu katika kazi zao kufuatia kutokuwepo kwa makubaliano ya kusimamisha mapigano kati ya jeshi la serikali ya Syria na kundi la upinzani jambo ambalo linamefanya kazi zao kuwa ngumu kwa kuhatarisha usalama wao.

Mahakama ya Kimataifa yapata mwanasheria mkuu Mwafrika.

Hague, Uhollanzi - 17/06/2012.  Mahakama ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu iliyopo nchini Uhollanzi imepata mwanasheria mkuu mpya wa mahakama hiyo.
Fatou Bensouda 51, aliapishwa kuwa mwanasheria mkuu wa mahakama hiyo siku ya Ijumaa 15/06/2012 ili kuchukua nafasi iliyo achwa na aliyekuwa mwanasheria mkuu wa mahakama hiyo Luis Moreno Ocampo ambaye ameachia madaraka hayo ambayo alikuwa anayashikilia tangu 2003.
Bi Fatou Bensouda mzaliwa wa Gambia alikuwa msaidizi wa Luis Moreno Ocampo tangu mwaka 2004 na amekuwa Mwafrika wa kwanza kushukuwa madaraka ya juu katika mahakama hiyo ya kimataifa tangu kuanzishwa.

Aung San Suu Kyi apokea zawadi yake ya Nobel.

 Aslo, Norway - 17/06/2012. Mwanaharakati, mwanasiasa na mtetezi wa haki za binadamu kutoka nchini Myanmar amezawadiwa zawadi Nobel ambayo alitunikiwa mwaka 1991.
Aung San Suu Kyi ambaye alikuwa amefungiwa kutoka katika nyumba aliyokuwa akiishi  kwa muda miaka 21 na serikali ya kijeshi ya nchi yake, alipokea zawadi hiyo jiji Aslo, na kutoa shukurani kwa wale tote waliokuwa muunga mkono wakati wa kifungo chake na kwa kuongeza kusema " zawadi hii ni changa moto na isiishie hapa bali iwe ufunguo kwa wale wote ambao wapefungwa na lazima waachiwe huru."
Aung San Suu Kyi, alishindwa kupokea zawadi hii ya Nobel mwaka 1991 kwa kuogopa ya kuwa akiondoka nchini huenda asiruhusiwe kurudi nchini mwake.

No comments: