Monday, June 18, 2012

Mazungumzo juu ya Iran na nyuklia yaanza nchini Urusi

Rwanda yafunga rasmi koti za Gacaca - Gachacha,


Kigali, Rwanda - 18/06/2012. Serikali ya Rwanda imefunga rasmi koti zilizo julikana kama Gachacha baada ya miaka 10 tangu zifunguliwe.
Mahakama hizo ambazo zilianzishwa ikiwa ni njia moja ya kutaka kuweka ukweli wa mauaji ya kikabila yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994.
Rais  Paul Kagame alitangaza rasmi kufungwa kwa mahamaka hizo na kutoa shukurani kwa wale wote walio   saidi katika kutafuta haki kwa Wanyarwanda wote.
Kwa mujibu wa serikari ya Rwanda zaidi ya watu 400,000 walifikishwa katika mahakama hizo ambazo mahakimu wake walikuwa  wameteuliwa na jamii kwa kuzingatia uwezo wao wa kupima mambo ya jamii.


Mazungumzo juu ya Iran na nyuklia yaanza nchini Urusi

Moscow, Iran - 18/06/2012.  Mazungumzo yameanza nchini Urusi ilikuzungumzia suala la kinyuklia la nchi ya Iran.
Mazungumzo hayo yanazikutanisha nchi za Iran, Urusi, Marekani, China, Ufaransa, Uingereza na Ujerumani kufuatia yale yaliyofanyika nchi Irak, ambayo haya kuleta jibu sahihi kuhusu Iran na mpango wake wa kinyuklia.
Catherine Ashton ambaye anawakilisha muungano wa nchi za Ulaya alisema " tutajitahidi kuongea na Iran ili iweze kukubaliana na jumuiya ya kimataifa kuhusu suala lake la kinyuklia."
Mazungumzo ambayo yanafanyika nchini Urusi yanatarajiwa kutoa utata  japo kuwa Iran, imesha tamka hapo awali kabla ya kuanza mazungumzo haya ya "kuwa hakutakuwa na mabadiliko juu ya haki nchi hiyo katika suala la kinyuklia kwani ni haki yake"kwani ni haki ya kila nchi

No comments: