Wednesday, June 13, 2012

NATO haina mpango wa kivita kwa nchi ya Syria.

Polisi wawakamata vinara wa vurugu jiji Warsaw.

Warsaw, Poland - 13/06/2012. Mamia wa wapenzi mchezo wa kandanda nchi Poland waliingiwa na mshangao baada ya washabiki kutoka nchi Urusi na Poland kupambana katika mitaa ya jiji la Warsaw.
Mashabiki hao walipambana kabla ya mmpambano kati ya timu ya taifa ya Urusi na Poland kuanza.
Msemaji wa polisi alithibitisha kukamtwa kwa watu 120 na watu zaid ya 10 waliumia vibaya.
Mashabiki hao walipambana kufuatia historia ya nchi hizi mbili, ambapo Urusi ilishawahi kuitawala Poland, jambo ambalo husababisha mvutano mkubwa kati ya nchi hizi mbili.

NATO haina mpango wa kivita kwa nchi ya Syria.

Sydney Australia - 13/06/2012. Katibu mkuu wa shirikisho la ulinzi la nchi za Ulaya na Amerika (NATO) ameagiza kuwepo na suruhusho la kisiasa nchi Syria.
Anders Fogh ambaye yupo ziarani nchi Australia alisema " Swala la Syria linabidi kusuruhishwa kimazungumzo  na NATO haita jiingiza kijeshi katika mgogoro wa Syria."
Katibu Anders Forgh yupo nchini Australia ili kuimarisha ushirikiano na nchi hiyo ambayo ni mshiriki wa NATO.

Jiji la Baghdad la kumbwa na milipuko.

Baghdad, Irak - 13/06/2012. Jiji la Baghdad limekumbwa na milipuko ya mabomu na kuu watu 57.
Mabomu hayo ambayo yalilipuka kwenye eneo linalo fanyika sherehe za hija za waumini wa dini ya Kislam wa Shia wakati walipokuwa wanatoa sadaka za vyakula na bidhaa nyingine.
Kundi linalo shirikiana na kundi la Al Qaeda lilipo nchini Irak limedai kuhusika na mashambulizi hayo

No comments: