Wednesday, August 26, 2009

Edward"Ted" Kennedy, Simba wa utetezi wa haki kwa watu wote, hatuko naye tena.

Edward "Ted" Kennedy, Simba wa utetezi wa haki kwa watu wote, hatuko naye tena.

Massachusetts, Amerika - 26/08/09. Kiongozi wa muda mrefu chama cha Demokratiki cha Amerika, Edward "Ted"Kennedy na ambaye amekuwa Seneta kwa kipindi kirefu amefariki leo kutokana na ugonjwa wa tarasani ya ubongo kwa muda mrefu.
Seneta,Ted Kennedy, alichaguliwa kuwa seneta wa Massachusetts mwaka 1962 kama senate na tangu hapo amekuwa seneta katika kipindi chote hicho.
Hata hivyo, atakumbukwa kwa kutaha haki kwa wa Amerika wote.
Hata hivyo, amehusika kwa ukaribu zaidi katika kampeni uchaguzi wa rais wa sasa Baraka Obama.
Picha hapo juu ni ya seneta, Edward "Ted" Kennedy, akiwa amesimama mbele ya ofisi za seneta, wakati wa uhahi wake.
Picha ya pili, wanaonekana, rais wa sasa wa Amerika, Baraka Obama kushoto , akiwa na hayati seneta Edward "Ted" Kennedy, akisikiliza kwa tabasamu baadhi ya maneno anayo sema, rais , Baraka Obama walipo kuwa pamoja katika moja ya mikutano ya chama cha Demokratik.
Jerusalemu ni ya Izrael, asema waziri mkuu Netanyahu.
London, Uingereza - 26/08/09. Waziri mkuu wa Izrael, Nenyamin Netanyahu, ameanza ziara ya bara la Ulaya , ili kuzungumza na viongozi wa bara Ulaya kuhusu swala zima hali ya Mashariki ya Kati.
Katika, ziara yake hiyo , amekutana na waziri mkuu wa Uingereza, Gordon Brown.
Wakati walipo kutana , waziri mkuu wa Izrael, alisema ya kuwa Jerusale, itakuwa mikononi mwa Izrael na haitakuwa chini ya Wapalstina na swala hili halina mjadara.
Katika ziara yake barani Ulaya, atakutana na kiongozi wa German na viongozi wengine.
Taliban yakili kifo cha kiongozi wao.
Waziristan ya Kusini,Pakistan - 26/08/09. Kundi la Taliban, limekubali ya kuwa kiongozi wao Baitullah Mehsud, amefariki dunia jana siku ya jumapili, kutokana na majeraha aliyo yapata baada ya mashambilizi yaliyo fanywa na ndege mtandao ya Amerika.
Kwa mujibu wa Taliban, Baitullah Mehsud, aliumia siku ya tarehe 05/08, baada ya ndege mtandao kushambulia nyumba ya baba mkwe wake.
Picha hapo juu ni ya , kiongozi wa Taliban eno la Waziristan Kusini, Baitullah Mehsud katikati, akiwa anawalinzi wake nyuma.
China yatoa ruhusa kuuza au kutoa viongo vya mwili kwa hiyari.
Beijing, China - 26/08/09. Serikali ya China, imetoa ruhusa kwa watu ambao kwa matakwa wapo tayari kutoa baadhi ya viongo vyao kwa ajili ya kusaidia watu wengine. Kwa mujibu wa serikali, shirika la msalaba mwekundu la China,kwa kusaidiana na wizara ya afya zitasimamia kwa uangalifu swala zima la hali hiyo.
Kufuatia kutolewa ruhusa hiyo, kutapunguza biaashara haramu ya ununuzi wa viungo vya binadamu ambayo ilikuwa inaanza kushamiri kwa sana.
Picha hapo, ni ya figo, kiungo ambacho huwa kina soko kubwa duniani.
Picha ya pili ni ya moyo, kiungo ambacho, upatikanaji wake umekuwa ni mgumu, lakini ikiwa mtu yoyote kabla ya kufariki, anaweza kutoa rai yake ni wapi moyo wake utumike.
Sigara kushutumiwa kuuwa watu zaidi ya millioni 6.
Washington, Amerika - 26/08/09. Shirika linalo shughulikia kuangalia afya za watu duniani, limesema yakuwa kiasi cha watu wapatao millioni 6, watapoteza maisha yao kutokana magonjwa yanayo sababishwa na uvutaji wa sigara, ifikapo mwisho wa mwaka ujao.
Kwa mujibu wa shirika hilo,(Lung Foundation), limesema yakuwa watu wengi watakao athirika ni wale wanao toka kwenye dunia ya tatu au nchi masikini duniani.
Zikithibitisha,habari kutoka kwenye shirika hilo zilimesema yakuwa uvutaji wa sigara katika nchi Amerika na za Ulaya hasa zile tajiri, uvutaji wa sigara umepungua kwa kiasi, lakini uvutaji wa sigara umeongezeka katika nchi masikini, na hivyo hali ya watu wengi kupoteza maisha kutokana na magonjwa yanayo sababishwa na uvutaji wa sigara kuongezeka.
Picha hapo juu, ni picha ya sigara, zao ambalo linachangia kuinua uchumi kwa kwa kuanzia wakulima na viwandani, lakini kwa upande mwingine, matumizi ya zao hilo kwa wateja wake ni ya kuathiri afya zao.

No comments: