Sunday, August 9, 2009

Viongozi wa siasa nchini Madagaska wakibaliana

Viongozi wa siasa nchini Madagaska wakubaliana kimsingi

Maputo, Mozambiki - 09/08/09. Vyama vya upinzani nchini Madagaska, vimekubaliana kushirikiana kuunda serikali ya mpito kwa kipindi cha miezi 15 chini ya usimamizi wa rais wa zamani wa Mozambiki, Joakim Chissano.
Kwa mujibu, wa msemaji wa UN (Umoja wa Mataifa) Tiebile Drame, pande zote mbili zimekubaliana kimsingi yakua kipindi hicho cha mpito cha miezi 15, kikifikia wanachi wa Madagaska, watajiandaa kupiga kura kwa uchaguzi mkuu.
Picha hapo juu, ni ya rais wa sasa wa Madagasca, Andry Rajoeli,ambaye aliingia madarakani, baada ya kung'olewa madarakani rais, Marc Ravalomanana.
Picha ya pili, ni ya rais wa zamani wa Madagaska, Marc Ravalomanana,ambaye kutolewa kwakwe madarakani watu wapato 100, walifariki dunia.
Picha ya tatu ni ya bendera ya Madagaska, nchi ambayo imekuwa na myumbo wa kisiasa tangu kufanyika mapinduzi yaliyo mng'oa madarakani rais, Marc Ravalomanana.

No comments: