Wednesday, August 12, 2009

Kura ya maoni ya Niger yaleta maswali kwa EU.

Kura ya maoni ya Niger yaleta maswali kwa EU.

Brussels, Ubeligiji - 12/08/09. Muungano wa nchi za Ulaya EU, umesema uhenda ikapunguza kuendela kuisaidia nchi ya Niger, baada ya rais Mamodou Tandja, kubadilisha katiba na kumwezesha kutawala tena kwa kipindi kingine.
Kubadilishwa kwa katiba hiyo ya nchi ya Niger, kumekuwa kukilaumuwa na nchi wanchama wa EU.
Mabadiliko hayo ya katiba, yatamwezesha rais Mamodou, kutawala kwa kipindi kingine cha miaka mitatu.
Picha hapo juu ni ya bendera ya nchi wanachama wa Muungano wa Ulaya, ambao umekuwa ikisaidia nchi ya Niger kwa muda mrefu.
Picha ya pili ni ya rais, Mamodou Tandja,ambaye kura za maoni zilikubali pendekezo lake.
Urusi kuimarisha jeshi lake karibu na mipaka na Georgia.
Sukhumi,Abhakazia - 12/08/09. Waziri kuu wa Urusi, Vladimir Putin, amesema ya kuwa nchi nyingi za Ulaya zinailaumu Georgia kwa kuanzisha vita,na viongozi Georgia hawataki kukubali ya kuwa wao ndiyo waliotoa mri ya kuanza vita.
Waziri mkuu yuho, Vladimir Putin,alisisi tiza kwa kusema yakuwa viongozi wa Georgia hawawezi kukubari kutokana na mkandamizo wanao upata kutoka Amerika.
Ziara hiyo katika jimbo la Abhakazia, ni katika kuangalia na kuwapa pole wale wote walio athirika na vita.
Waziri mkuu, Putin, alisema Urusi itawekeza $ 470, ili kuimarisha ulinzi katika eneo la Abhakazia na kipaka na Georgia.
Picha hpo juu, anaonekana mama , mmoja alimsalimia waziri mkuu, wa Urusi, Vladimir Putin, alipo tembelea Abhakazia.
Rais atoa amri kutafutwa kwa meli iliyo potea.
Moscow, Urusi -12/08/09. Rasi wa Urusi, Dmitry Medvedev, ametoa amri ya kutafutwa kwa moja ya meli ya mizigo iliyo potelea karibu na pwani ya Ufaransa.
Kwa mujibu wa msemaji wa idara ya ulinzi wa bahari wa Urusi,Vladimir Vysotsky,alisema amri hiyo,imekuja mara baada ya juuudi za kutafuta meli hiyo kuleta utata.
Meli hiyo iliyo kuwa na raia wa Urusi, ilipotelea njiani tangu tarehe 4/8/09, njiani kuelekea Algeria.
hata hivyo kuna wasiwasi yakuwa meli hiyo,huenda ikawa imetekwa na na maharamia.
Picha hapo juu ni rais wa Urusi, Dmitry Medvedev , ambaye ameagiza kutafutwa kwa meli iliyopotelea baharini.

No comments: