Wednesday, August 5, 2009

Mahmoud Ahmadinajed, aapishwa tena kuwa rais wa Iran.

Billy Clinton, azuru Korea ya Kaskazini, waandishi wa habari wa achiwa huru.

Los Angeles,Amerika - 05/08/09. Waandishi wa habari wawili raia wa Amerika, Laura Ling na Euna Lee,wameachiwa huru na kuwasili nyumbani kuungana na familia zao, baada ya kukaa jela kwa muda wa miezi minne na siku kadhaa kwa msamahaa wa rais wa Korea ya Kaskazini.
Kuchiwa kwao kumekuja mara baada ya rais wazamani wa Amerika,Billy Clinton kufanya ziara ya ghafla nchini Korea ya Kaskazini, na kuongea na rais Kim Jong Il.
Hata hivyo hakuna habari zozote zilizo elezwa kuwa viongozi hawa waliongea nini.
Picha hapo juu, wanaonekana, rais wa zamani wa Amerika, Billy Clinton kushoto,na rais wa Korea ya Kaskazini, Kim Jong Il, wakati alipo kuwa nchini Korea ya Kaskazini.
Picha ya pili, wanaonekana, Laura na Euna, wakishuka kutoka kwenye ndege, kukanyaga ardhi ya Amerika, baada ya kuachiwa huru kwa msamahaa wa rais wa Korea ya Kaskazini.
Picha ya tatu, wanaonekana, Laura na Euna wakikaribishwa kuingia kwenye ndege na rais wa zamani wa Amerika Billy Clinton.
Mahmoud Ahmadinajed, aapishwa tena kuwa rais wa Iran.
Tehran,Iran - 05/08/09. Mahmoud Ahmadinejad ameapishwa kwa mara ya pili kuwa rais wa Iran.
Akiongea baada ya kuapishwa, rais, Mohmoud Ahmadinejad,alisema ya kuwa atafanya mabadiliko katika serikali yake, kitaifa na kimataifa.
Katika, sherehe ya kuapishwa kwake, kuliudhuliwa na viongozi na mabalozi wa nchi tofauti, lakini baadhi ya viongozi wa vyama pinzani walisusia sherehe hiyo.
Picha hapo juu, anaonekana,rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad kulia,akikabidhiwa hati za serikali na kiongozi mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei aliyepo kushoto.
Picha ya chini, anaonekana, rais wa Iran,Mahmoud Ahmadinejad,akiongea mara ya baada kuapishwa kwake.

No comments: