Saturday, August 29, 2009

AQ Khan ruhusa kutembea,kizuizi cha ondolewa.

Matuzi ya madawa tofatuti ndiyo chanzo cha kifo cha mfalme wa musiki wa pop.

Los Angeles,Amerika - 29/08/09. Wachunguzi wa kisayansi ambao walikuwa wanachunguza kifo cha aliyekuwa mfalme wa musiki wa pop, Michael Jackson, wamesema yakuwa kifo chake kilisababishwa na madawa ambayo alikuwa amemeza kwa ajili ya matibabu.
Baada ya uchunguzi wa mfalme huyo wa musiki wa pop, hayati Michael Jackson,kufanyika, alikutwa na na madawa ya aina ya midazolam,diazepam, au Valium; lidocaine,alocal anesthetic;na ephedrine.
Hata hivyo polisi , L.A .P.D., imesema bado wanaendelea na uchunguzi zaidi.
Picha hapo juu ni ya hayati, Michael Jackson, aliyekuwa binngwa na mfalme wa musiki wa pop,akiwa punguia mikono wapenzi wa muziki walio kuja kumuona enzi ya uhai wake.
Picha ya pili, anaonekana hayati, Michael Jackson, mfalme wa muziki wa pop, akitumbwiza jukwaani.
Meli ya siraha kutoka Korea ya Kaskazini ya kamatwa.
Dubai,UAE,- 29/08/09. Serikali ya Muungano wa nchi za Kiaraab, imesema ya kuwa imeikamata meli ya mizigo ambayo ilikuwa imebeba siraha kutoka Korea ya Kaskazini.
Habari kutoka serikali ya UAE zimesema, meli hiyo ya mizigo ilikuwa imebeba siraha zilizo kuwa zikielekea Iran.
Kwa mujibu wa habari hizo, ambazo zilipelekwa umoja wa Mataifa,na baadaye barua kutumwa Korea ya Kaskazini na Iran, zilisema UAE, ilikamata meli hiyo, kutekeleza sheria ya umoja wa mataifa wa kuiwekea vikwazo Korea ya Kaskazini.
Meli hiyo, ilikamatwa tarehe 14/08/09, ikiwa na siraha tofauti zilizobebwa na meli ya shirka la meli la Australia ANL.
Picha hapo juu, ni ya meli iliyo kamatwa na serikali ya UAE, ikiwa na siraha kutoka Korea ya Kaskazini.
AQ Khan ruhusa kutembea, kizuizi cha ondolewa.
Lahore,Pakistan - 29/08/09. Mwana sayansi ambaye anadaiwa ndiye kiini cha nchi ya Pakistan kupata sayansi ya utengenezaji wa nguvu za kinyuklia Abdul Qadeer Khan, amepewa ruhusa ya kuwa rais huru na mahakama.
Ruhusa hiyo ilitolea baada ya, AQ Khan kukata rufaa kwa kudai ya kuwa ilikuwa ni kinyume cha sheria ya yeye kuzuhiliwa kuwa huru kama mwanchi mwingine wa Pakistan.
AQ Khan,aliwekwa kizuizini na serikali ya aliye kuwa rais wa Pakistan, Pervez Musharaf, baada ya ushaidi kuonyeha alihusika katika biashara ya kuuza utaalaamu wa sayansi ya nuklia kinyume cha sheria kwa nchi za Libya, Iran na Korea ya Kaskazini.
Picha hapo juu,ni ya AQ Khan, ambaya ameruhusiwa kuwa huru.
Rais, Jakob Zuma, asisitiza uhusiano na ushirikiano wa serikali ya Zimbabwe.
Harare, Zimbabwe - 29/08/09. Rais wa Afrika ya Kusini, Jakob Zuma, amewataka viongozi wa serikali ya Zimbabwe kushirikiana ili kujenga nchi yao.
Rais , Zuma , alisema ya kuwa umefika wakati wa viongozi wa serikali ya Zimbabwe kuweka siasa pembeni, kufikiria na kufikiria ni kwa jinsi gani watainua uchumi wa nchi na kutimiza yale walio kubaliana wakati walipo saini mkataba mapema mwezi february..
Picha hapo juu wanaonekana, rais wa Zimbabwe Robert Mugabe kushoto, akiwa na rais wa Afrika ya Kusini Jakob Zuma wakati walipo kutana mjini Harare.
Korea ya Kusini na Kaskazini zafanya mazungumzo ya karibu.

Seoul, Korea ya Kusini - 29/08/09. Viongozi wa serikali za Korea ya Kusini na ya Kaskazini wamekutana hivi karibuni ili kujadili hali halisi ya maeneo ya nchi zao

Mazungumzo hayo , ambayo yanafanyika karibu na mlima wa Kumgang,yanalenga hasa ni jinsi gani nchi hizi zitashirikiana katika kuungani familia zilizo tengana tangu mwaka 1950, baada ya vita kuisha kati ya nci hizo.

Kwa mujibu wa habari, kuna watu wapatao 600,000 kutoka Korea ya Kusini waliopo Korea Kaskazini,ambao hawajawahi kuonana na ndugu zao tangu miaka ya 1950.

Picha hapo juu, wanaonekana viongozi wa Korea ya Kaskazinia na Kusini wakisaliamiana wakati viongozi hao walipo kutana kujadili hali halisi ya nchi zao.

2 comments:

Anonymous said...

Hello, just ωanted tο ѕay, I enjoуed thiѕ article.
It was іnsρiring. Keep on poѕtіng!


Alѕо vіsіt my site .

.. http://www.netsurfquiz.com
Here is my page ... Pay Day Loans

Anonymous said...

If you woulԁ like to οbtain a good ԁeal fгοm thiѕ parаgraph then you haѵe to apply theѕe technіques to your wоn weblog.


Сhесk out my pagе; Payday Loans Online No Credit Check
my website > Payday Loans