Rais wa za zamani wa Zambia, ashukuru Mungu, "Kesi imefutwa"
Lusaka, Zambia - 19/08/09. Rais wa zamani wa Zambia, Frederick Chiluba, ameachiwa huru, baada ya kukutwa hana hatia ya kula rushwa wakati wa uongozi wake akiwa rais wa Zambia.
Kesi hiyo, ambayo aliyo kuwa inamkabiri rais huyo wa zamani wa Zambia, Fredrick Chiluba ni kuhusika na upotevu wa $500,000 za Amerika
Kwa mujibu wa mahakama, wanasheria wa serikali walio fungua kesi hiyo walikosa ushahidi kamili.
Rais huyo wa zamani wa Zambia, Fredrick Chiluba, amekuwa akikabiliwa na kesi iliyo chukuwa miaka minane tangu ashitakiwe.
Mungu ni mkubwa, ameonyesha ukweli upo wapi na alisikika akisema hayo rais huyo wa zamani wa Zambia.
Picha hapo juu, anaonkekana, rais wa zamani wa Zambia, Fredrick Chiluba, akinyanyua mikono juu kumshukuru Mungu, mara ya kusikia kesi iliyo kuwa ikimkabili imetupiliwa mbali na mahakama.
Wanaume wabakwa kwa wingi nchini DRC.
Goma, DRC - 19/08/09. Hali imezidi kuwa mbaya katika eneo la Goma, baada ya wanaume kuanza kubakwa.
Kwa mujibu wa mmoja ya watu waliokumbwa na mkasa huo,Kazungu Ziwa,alisema alivamiwa na kukamatwa na watu wenye mapanga na virungu.
Baada ya kuvamiwa alijaribu kupigana nao, lakini alishindwa , na matokeo ya ke wakamtawiti kwa nguvu, na baadaye walimwacha akiwa taabaani.
Kwa mujibu wa bwana Ziwa, alisema ya kuwa watu hao, walikuwa ni moja ya makundi wanaopigana katika maeneo hayo.
Picha hapo juu, ni moja ya picha za watu ambao walikumbwa na mikasa ya kulawitiwa.
London,Uingereza -19/08/09.Mmoja wa wataalamu wanaofatilia tiba ya kansa,Ine Diaz-Laviada, amesema ya kuwa mmea wa bangi unaweza kusaidia kuponyasha ugonjwa wa kansa.
Nairobi, Kenya - 19/08/09. Raia wa Kenya, Mzee, Kimani Nganga Maruge aliyekuwa na miaka 90, amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa kansa ya tumbo.

No comments:
Post a Comment