Friday, August 21, 2009

Usain Bolt, hana mpinzani katika mbio za mita 100 na 200.

Usain Bolt, hana mpinzani katika mbio za mita 100 na 200.

Berlinn Ujerumani - 21/08/09. Usain Bolt, mwana riadha wa Jamaika, amevunja rekodi za dunia za mbio za mita 100 na 200 kwa upande wa wanaume.
Usain Bolt,ambaye amekuwa hana mpinzani, aliwashangaza wapenzi wa riadha, na kuwaacha macho yakiwa hawaamini ya kuwa rekodi ya mbio za mita 200 ya sek 19:32, iliyo wekwa na Michael Johnson, baada ya kukumbia mbio hizo za mita 200 kwa sek 19:19.
Picha hapo juu,anaonekana, Usain Bolt, akiwa mbele pekee yake mara baada ya kuvuka mstari wa mwisho, na kuvunja rekodi.
Picha ya pili, anaonekana, Usain Bolt, akiwa mbele ya wakimbiaji wenzake wakati wa fainali za mita 200.
Picha ya tatu, anaonekana, Usain Bolt, akiwa mbele ya tangazo, linalo onyesha ya kuwa ameweka rakodi mpya ya dunia ya mbio za mita 200.
Mtuhumiwa wa Lockerbie awasili nyumbani.
Tripol, Libya -21/08/09. Abdel Basset al Megrahi,ambaye anatuhuniwa kwa kuhusika na mlipuko wa bomu nadni ya ndege ya Pan Am 103, amewasili nyumbani, baada ya kuachiwa huru jana na serikali ya Uingereza, kwa kuzingatia hali ya afya yake.
Bwana, Abdel Basset al Megrahi, alikuwa amehukumiwa kifungo cha maisha, mara baada ya kukutwa na hatia ya kuhusika na ulipuaji wa ndege iliyo kuwa imebeba watu 270, watu wote kupoteza maisha kutokana na mlipuko huo.
Kufuatiwa kuachiwa kwake, baadhi ya viongozi wa kimataifa wamekuwa wakitoa maoni tofauti,kuhusu kuachiwa kwake.
Lakini hata hivyo, Abdel Basset al Megrahi, alipokelewa kwa shwange alipo wasili jijini Tripol.
Picha hapo juu, anaonekana, akiwa ameshikiliwa na baadhi ya watu waliokuja kumpokea.
Picha ya pili, anaonekana A.B. al Megrahi,akipanda ngazi kuingia ndani ya ndege, tayari kuanza safari ya kurudi nyumbani Libya.
Picha ya tatu, A.B.al Megrahi, akishuka kutoka kwenye uwanja wa ndege nchini Libya na wanaonekana mamia wakija kumpokea kwa shangwe.

No comments: