Monday, August 10, 2009

Uingereza haitaruhusu watu kuteswa na makachero.

Wepesi wa mawasiliano ya kimtandao kuwepo Afrika. Mombasa, Kenya - 10/08/09.Kampuni ya SEACOM, imewekeza kiasi cha $ 2.6billion katika eneo la Afrika ya Mashariki katika kuinua mawasiliano ya kimtandao. Kwa mujibu wa mtasmini wa mambo ya mawasiliano, David Lerche, alisema ya kuwa Afrika itafaidika kwa kiasi kikubwa zaidi ya mara 10, na kuweza kuwasiliana na mabara mengine kiuraisi zaidi kwa kutumia mtandao, kwani mitambo hiyo itaunganisha bara la Asia na Ulaya na itakuwa na nguvu zaidi. Picha hapo juu wanaonekana, wafanyakazi wa kiwa kazini kuvuta moja ya waya za kupitishia mawasiliano katika mji wa Mombasa nchini Kenya kuelekea ndani ya bahari ya Indi kuelekea katika bara la Asia. Uingereza haitaruhusu watu kuteswa na makachero. London,Uingereza, 10/08/09.Serikali ya Uingereza, imesema yakuwa itakuwa ni vigumu, kwa makachero au majasusi wa nchi kukubali au kukataa ya kuwa habari zilizo patikana, lizipatikana kutoka kwa watu washukiwa wa makundi ya uhaini, baada ya kuteswa kwa kinyume cha sheria za haki za binadamu. Akiongea hayo, waziri wa mambo ya nje wa Uingereza, David Miliband, alisema hayo alipo kuwa akiongea na vyombo habari, na kusema ya kuwa serikali ya Uingereza, hairuhusu wa kutesa watu kwa aajili ya kupata habari na hii ni kinyume na haki za binadamu. Picha hapo juu ni ya waziri wa mambo ya nje wa Uingereza, David Miliband,alipo kuwa akiongea na vyombo vya habari siku ya jumapili wiki hii. Uhusiano wa Venezuela na Kolombia wawa wa wasiwasi. Caracas, Venezuela - 10/08/09. Rais wa Venezuela, Hugo Chavez, amekaripia nchi ya Kolombia kwa kudai yakuwa imetuma wanajeshi kuingia Venezuela. Akisisitiza ,rais Hugo Chavez, alisema ya kuwa hawakuwa askari wa kulinda mpaka, bali walikuwa ni wanajeshi na walivuka Mto wa Orinoco na kuingia hadi ndani ya Venezuela. Na wakati wanjeshi wa Venezuela walipokwenda kwenye eneo hili, walikuta wanajeshi wa Kolombia wamesha ondoka. Venezuela, imekua ikipinga kitendo cha Kolombia kuruhusu, Amerika kuweka kambi zake za kijeshi nchini Kolombia. Na wakti huo huo , Kolombia imekuwa ikiilaumu Venezuela, kwa kuwasaidia waasi wa kundi la FARC, ambalo linapingana na serikali ya Kolombia. Hata hivyo, serikali ya Kolombia imekanusha madai hayo. Picha hapo juu, wnaonekana, rais wa Venzuela, Hugo Chavez, akiongea na vyombo vya habari.

No comments: