Thursday, August 20, 2009

Uchaguzi wa Afghanistan, wakamilika jumuia ya kimataifa yangoja matokeo yake
Kabul, Afghanistan - 20/08/09. Wanachi wa Afghanistan, wamemaliza kupiga kura kuwachagua viongozi watakao ongoza nchi kwa kipindi cha miaka mitano mingine.
Kufuatia kumalizika kwa kupigwa kwa kura leo 1700( saa kumi na moja) kwa masaa ya Afghanistan, kura zimeanza kuhesabiwa rasmi. Kumalizika kupiga kura nchini Afghanistan, kumesifiwa na mwakilishi wa serikali ya Amerika, Richard C Holbrooke.
Bwana, Holrbooke, alisema ya kuwa wanchi wa Afghanistan, wameweza kupiga kura bila kuogopa vitisho vya Taliban, na huu ndiyo mwanzo wa kuijenga nchi yao Waafghanistan.
Picha hapo juu ni za wagombea wa kiti cha urais wa Aghanistani, kutoka kushoto,Abdullah Abdullah,Ramadhani Bashardost, Ashraf Ghani na Hamid Karzai.
Picha ya pili, wanaonekana wanchi wa Afghanistan, wakiwa katika mstari tayari kupiga kura kuchagua viongozi wao.
Uingereza yatakiwa kudhibiti biashara ya siraha.
London, Uingereza 20/08/09.Shirika linalo shughulikia usimamizi wa uuzaji wa siraha duniani, limeitaka serikali ya Uingereza, kuchukua hatua upya ya kusimamia reseni na uuzaji wa siraha wa makampuni yanayo uza siraha hizo ambazo zinatikea nchini humo.
Kwa mujibu wa shirika hilo,limesema yakuwa, katika uchunguzi wake, limegundua ya kuwa siraha nyingi zinazo tumika katika mapigano sehemu tofauti zinaalama ya matengenezo kutoka Uingereza.
Shirika hilo pia limeitaka serikali ya Uingereza kujaribu kushirikiana na mashirika ya siyo ya kiserikali ili kudhibiti uuzaji haramu wa siraha hizo.
Hata hivyo serikali ya Uingerza imesema yakuwa inafuata sheria za kimataifa na itazidi kuimarisha udhibiti huo.
Picha hapo juu ni ya bendera ya Uingereza nchi ambayo imetakiwa kuongeza bidii kudhibiti uuzaji wa siraha zinazo tokea nchini humo.

No comments: