Tuesday, February 1, 2011

John Kerry ataka rais wa Misri kuachia madaraka. New York, Marekani - 01/02/2011. Mbuge na kiongozi muhimi katika chama cha Demokratik cha Marekani amemtaka rais wa Misri kujiudhuru.

John Kerry alisema " Mubaraka lazima akubaliane na matakwa ya wananchi na raia wa Misri kwa ajili ya usalama na kulinda hadhi ya Wamisri na mtoto wake asigombanie kiti cha urais wakati wa uchaguzi, pia Marekani inatakiwa kuangalia mbele na kujua ya kuwa kipindi cha Mubaraka kimekwisha."
John Kerry amekuwa kiongozi wa kwanza wa ngazi ya juu kutoka Marekani kutamka wazi ya kuwa rais Mubaraka aachie madaraka.
Picha hapo juu ni ya mbuge John Kerry, ambaye amekuwa wa kwa kutamka wazi kuwa rais wa Misri Hosni Mubaraka atoke madarakani.
Rais wa zamani wa Haiti kurudi nyumbani.
Port au Price, Haiti - 01/02/2011.Serikali ya Haiti imekubali kumpa kibali cha kurudi nyumbani aliye kuwa rais wa nchi hiyo ambaye alikimbilia Afrika ya Kusini.
Jeans Bertrand Aristide aneyeishi ukimbizini nchi Afrika ya Kusini amekuwa akisema kila mara yupo tayari kurudi nyumbani ikibidi kufanya hivyo.
Ira Kurzban, mwanasheria wa wa Aristide amesema " ninacho fahamu ni kwamba rais Jeans Bertrand Aristide amepewa pasipoti tayari kurudi nyumbani na kamati ya serikali ya Haiti."
Kurudi kwa Aristide kutakaribiana na uchaguzi wa mara ya pili wa kumchagua rais wa Haiti ambao utafanyikahivi karibuni.
Picha hapo juu ni ya rais wa zamani Jean Bertrand Aristide ambaye anatarajiwa kurudi nyumbani kutoka ukimbizini.
Mfalme wa Jordani avunja serikali.
Aman Jordan - 01/02/2011. Mfalme wa Jordani amevunja serikali baada ya kushindwa kuimarisha uchumi wa nchi na kusababisha wananchi kuandama.
Maandamano hayo ambayo yamefanyika zaidi ya wiki, yalianza baada ya kupanda kwa mafuta na bei ya vyakula.
Habari kutoka ofisi ya mfalme zinasema " mkuu wa jeshi wa zamani Marouf Bakhit ambaye aliyewahi kuwa waziri mkuu hapo awali amechaguliwa kuwa kuunda serikali mpya baada ya serikali ya Samir Rifai kushindwa kuimarisha uchumi."
Wananchi wa Jordan wamekuwa wakilalamikia serikali kwa kushindwa kuimarisha uchumi na kusababisha maisha ya raia kuwa magumu.
Picha hapo juu ni ya Mfalme wa Jordan ambaye amevunja serikali baada ya kushindwa kuongoza wananchi na kuinua uchumi Jordan.

No comments: