Friday, February 18, 2011

Milipuko yatokea nchini Tanzania

Milipuko yatokea nchini Tanzania

Dar es Salaam, Tanzania - 18/02/2011. Milipuko ya mabomu imeua zaidi ya watu ishirini na kuleta maafa makubwa kwenye kambi moja ya jeshi iliyopo nje kidogo ya jiji la Dar es Saalam.
Mlipuko huo ambao ulitokea usiku wa kuamkia Jumatano na kusababisha wenyeji wa maeneo hayo kukimbia mji wao kwa uwoga.
Milipuko hiyo iliyo tokea katika kambi ya jeshi iliyolo Gongo la Mboto wilaya ya Ilala imesababisha maafa makubwa kwa jamii.
Mizengo Pinda alisema " milipuko hiyo imeleta maafa makubwa na huenda baadaye maafa yakaongezeka kutokana na hali halisi iliyo sababishwa na milipuko hiyo."
Milipuko ya mabomu katika kambi ya jeshi la Gongo la Mboto imetokea kwa mara ya pili baada ya milipuko uliyo tokea mwaka 2009 ambapo watu wapatao 27 walipoteza maisha yao.
Wamisri washangilia wiki moja tangu kuondoka Hosni Mubaraka.
Kairo, Misri - 18/02/2011. Maelfu ya wananchi nchini Misri wameandamana ili kushangilia kuanguka kwa utawala wa Hosni Mubaraka.
Rais Hosni Mubaraka ambaye alikuwa rais wa Misri kabla ya kuamua kuachia madaraka baada ya wanachi kuandamana kutaka serilikali ya Mubaraka iachie utawala.
Hata hivyo kulikuwa na maandamano mengine yalifanyika katika jiji la Kairo kuunga mkono Hosni Mubaraka kwa madai ameiniua nchi na kuleta amani.
Rais Hosni Mubaraka, alitoka madarakani baada ya maandamano ya siku kumi na nane ambayo yalimlazimisha kuachia madaraka ya urais.

No comments: