Saturday, February 26, 2011

Umoja wa mataifa kuwekea vikwazo serikali ya Libya.

Umoja wa mataifa kuwekea vikwazo serikali ya Libya. New York, Marekani - Kamati ya usalama ya umoja wa Mataifa imekutana ili kujadili muswada wa kuiwekea vikwazo serikali ya Libya.

Uamuzi huo wa umoja wa mataifa umekuja baada ya serikali ya Libya chini ya kiongozi wa nchi hiyo Muammar Gaddafi kutumia nguvu kuvunja maandamano ambayo yanapinga serikali yake.
Kwa mujibu wa habari kutoka katika kamati hiyo ya umoja wa mataifa zinasema " serikali ya Libya inatumia nguvu zake za dola kimyume na kusababisha vifo na maafa katika jamii nzima ya Walibya."
Hali ya kiusalama nchini Libya imebadilika na kuwa uwanja wa vita mara baada ya maandamano ya kumtaka kiongozi wa nchi hiyo Muammar Gaddafi kutika madarakani jambo ambalo kiongozi huyo amekataa.
Picha hapo juu anaonekana kiongoziwa Libya Muammar Gaddafi akiwahutubiwa wananchi kwa mara ya tatu tangu kuanza maandamano ya kumtaka aachie madaraka.
Hali ya kuzuka vita vya wenyewe kwa wenyewe huenda ikatokea.
Abidjani, Ivory Coast-26/02/2011. Milio ya risasi imesikika katikati ya jijila Abidjani na kuwafanya wakazi wake kukimbia kwenye maficho huku katibu mkuu wa umoja wa mataifa akionya kuibuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.
Mapigano hayo ambayo yalikuwa kati ya kundi la rais wa sasa wa nchi hiyo Laurence Gbagbo na Alassane Ouattara.
Kwa mujibu wa habari zilizo patikana zimasema " halisiyo shwali katika jiji hilo."
Hali ya machafuko ilianza mara baada ya uchaguzi mkuu kufanyika na Gbagbo kudai yeye ndiye aliye shinda uchaguzi na huku mpinzani wake Ouattara kudai yeye ndiye mshindi wa uchaguzi huo.
Picha hapo juu ni viongozi wa makundi yanayo pigana nchini Ivory Coast, Watara kushoto na Gbagbo kulia

No comments: