Sunday, February 13, 2011

Rais wa zamani wa Pakistani ashitakiwa.

Kiongozi wa Palestina ajiudhulu kazi yake. Ramallah, Palestine - 13/02/2011. Msemaji mkuu wa serikali ya Wapalestine amejiudhulu katika kazi yake baada ya habari zilizo patikana kwenye vyombo vya habari zimetokea kwenye ofisi yake. Saeb Erakat, ambaye amekuwa msemaji mkuu wa serikali ya Wapalestina kwa muda mrefu, amekuwa akiandamwa na mlolongo wa lawama ya kuwa amekuwa hafanya kama anavyotakiwa hasa katika majadiliano ya kuleta amani na Waizrael. Habari ambazo zilipatikana kwenye vyombo vya habari hivi karibuni zimeonyesha jinsi gani viongozi wa Palestina wanavyo jadiliana katika majadiliano ya amani na Waizrael ambayo yamesimama kutokana na tofauti za misimamo. Rais wa zamani wa Pakistani ashitakiwa.

Islamabad, Pakistan - 13/02/2011. Mahakama nchini Pakistan imetoa kubali cha kumtaka aliyekuwa rais wa zamani wa nchi hiyo kukamatwa ili ajibu mashitaka ya kuwa alihusika na mauaji ya aliyekuwa waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo.
Musharaff, ambaye alikuwa rais wa Pakistan na amiri jeshi mkuu wa nchi hiyo, anatuhumiwa kwa kuhusika na mauaji ya aliyekuwa waziri mkuu Benazir Bhutto.
Habaria kutoka kwa viongozi wa serikali zinasema " uchunguzi ulio fanywa unaonyesha kwa njia mojo au nyingine uongozi wa serikali ya Musharaff uliyo kuwepoe wakati wa mauji ya Benazir Bhutto unahusika."
Hata hivyo, upande wa Musharaff unakanusha madai hayo na kusema ni habari za uvumishi ndizo ambazo zimetumika na Musharaff hausiki na mauaji hayo.
Pervez Musharaff anatarajiwa kuwasili mahakamani tarehe 19 Februari 2011 ilikusikiliza kesi dhidi yake.

No comments: